Tetesi zinasema, Chelsea wanafikiria uwezekano wa kumnunua beki wa Leicester na Ufaransa wa chini ya umri wa miaka 21 Wesley Fofana, 20, Antonio Rudiger, 28, na Andreas Christensen, 25, wakiwa bado hawajasaini kandarasi mpya Stamford Bridge.
Tetesi zinasema, Newcastle United, Barcelona, Arsenal na Paris St-Germain wanaongoza katika kinyang’anyiro cha usajili wa mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial, 26.

Tetesi zinasema, Rais wa Barcelona Joan Laporta anasema klabu inaelekea katika mwelekeo sahihi na kikosi cha kwanza kitaimarishwa katika dirisha la uhamisho la Januari.
Barcelona wameongeza dau lao la kumnunua winga Mhispania wa Manchester City Ferran Torres,21, kwa hadi euro miliomi 45 sawa na (£38m) Pamoja na malipo mengine ya ziada ya euro milioni 15 sawa na (£12.8m).
Barcelona pia wanamnyatia mshambuliaji wa River Plate na Argentina wa miaka 21 Julian Alvarez, ambaye ana kifungu cha kuuzwa kwa euro milioni 25 sawa na (£21.3m).
Tetesi zinasema, Kiungo wa Wales, Aaron Ramsey anataka kuondoka Juventus ifikapo Januari mwakani, huku Everton na Newcastle zikionesha nia ya kutaka kumnunua mchezaji huyo wa miaka 30.

Manchester City wanamtaka beki wa Arsenal Mreno Nuno Tavares, 21, ambaye ameonyesha uwezo mkubwa uwanjani tangu alipojiunga na klabu hiyo msimu wa joto kutoka Benfica.
Tetesi zinasema, Arsenal wako tayari kulipa euro milioni 80 (£68m) kumpata mshambuliaji wa Fiorentina’s na Serbia Dusan Vlahovic,21.
Unaweza kujishindia mamilioni katika kasino yako pendwa ya meridianbettz, mchezo wa Agent Jane Blonde Return ni moja ya michezo inayopendwa kwasasa huku ikiwafanya wachezaji kuwa mamilionea kila siku. Unasubiri nini! ungana na Agent Jane Blonde akufanye milionea.
CHEZA HAPA


