Klabu ya Cardiff City imepata onyo zito kutoka FIFA kwamba wanatakiwa kuwalipa Nantes ada ya uhamisho wa Emiliano Sala ambayo kiwango cha £5.3m endapo klabu hiyo itashindwa kulipa pesa hiyo itakutana na adhabu ya kufungiwa kusajili kwa kipindi cha miaka mitatu na adhabu nyingine.
Manchester City wamewashauri Real Madrid kusahau ndoto yao ya kufikiri kwamba wanamsajili Raheem Sterling hivi karibuni. Wamewaambia kwamba hiyo ndoto haina manufaa kwa sababu hawana mpango huo na kwao wanachukulia jambo hilo kuwa halina namna inavyowezekana hivi karibuni.
Manchester United bado wanalifikiria ombi la Roma juu ya uhitaji wao kumsajili moja kwa moja nyota wao lakini wakiwataka waongeze kiasi hicho cha fedha kama wanamaanisha kweli kuifanya biashara hiyo na klabu yao. Mapema Roma waliwasilisha ombi lao la kumtaka nyota huyo asalie klabuni hapo kwa mkataba wa kudumu.
Chelsea wamewajumuisha kwenye hesabu zao nyota wa klabu ya Crystal Palace, Wilfred Zaha na nyota wa Leipzig, Timo Werner juu ya nia yao ya kuwasajili nyota hao kama watapewa kibali cha kusajili. Japo kocha wa klabu hiyo, Frank Lampard anasema hata kama watazuiliwa kusajili hawana wasiwasi maana kwa nafasi fulani amefanikiwa kuwajenga wachezaji aliokuwa nao klabuni hapo kwa sasa.
Fenerbahce wapo mbioni kufukuzia saini ya nyota wa klabu ya Chelsea ambaye mkataba wake wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo upo mwishoni kwa sasa. Pedro amekuwa na kikosi cha Chelsea kwa muda sasa na anaangalia namna ya kuachana na klabu yake hiyo endapo atapata klabu ya kuichezea kwa majira ya hapo mbeleni.
Nyota wa Salzburg, Haaland ana ndoto kubwa ya kuichezea ligi ya Uingereza siku za mbeleni. Baba mzazi wa nyota huyo anadai kwamba mwanaye ana ndoto kubwa sana ya kusonga mbele kwenye soka lake.
Mlinda mlango wa Sheffield United, Henderson ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo anasema alikaribia kujiunga na klabu ya Leeds pindi alipotokea katika klabu ya Manchester United. Nyota huyo kwa sasa anakipiga na klabu hiyo akiwa na kiwango ambacho hakina upinzani ndani ya klabu hiyo.
Povel
Habar njema