Tujikumbushe: Kichwa cha Zidane kwa Materazzi Kombe la Dunia 2006

Pengine Juni 13 2006 ni siku iliyobeba kumbukumbu mbaya kwa Mkongwe wa soka Zinedine Yazid Zidane ‘Zizzou’,  lakini siku hiyo ina kumbukumbu mbaya zaidi kwa mkongwe mwingine wa soka la Italia Marco Materazzi, nitakwambia kwa nini.

Siku hiyo ni siku ambayo ulimwengu wa soka ulishuhudia mchezo wa fainali ya kukata na shoka kati ya miamba miwili ,yani Ufaransa dhidi ya Italia. Ufaransa waliingia wakiwa wamepewa nafasi ya kushinda mechi hiyo na kuubeba ubingwa  huo hasa kutokana na ukubwa wa majina waliyokua nayo katika kikosi. Hivi unatokaje mbele ya timu yenye Thiery Henry, Eric Abidal na William Gallas? Kama unafikiri haiwezekani,  niambie utafikiria nini baada ya kuambiwa kikosi hicho pia kilikuwa na Claude Makelele, Frolent Malouda, Frank Ribery na fundi mwenyewe Zinedine Zidane! Ufaransa walikamilika bwana.

Lakini kama unavyojua, katika soka halitokei jambo kabla halijatokea. Ufaransa waliambulia kupata sare ya kufungana goli moja kwa moja, na baadae wakapoteza katika changamoto ya mikwaju ya penati mbele ya ‘watukutu’ wakina Cannavaro, Grosso,  Andrea Pirlo na wenzao wa Italia.

Zidane hawezi kuisahau hii siku kwa kuwa ndiyo ilikua siku aliyocheza mechi yake ya mwisho akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa. Kama hilo halitoshi kumfanya asiisahau hii siku basi ataikumbuka kwa kuwa ni siku ambayo licha ya kuwa walipoteza dhidi ya wapinzani wao yeye alipewa heshima ya kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano. Hilo nalo likimfanya asiikumbuke siku hiyo basi atajiwe jina ‘Materazzi’,  hapo kumbukumbu zake zote juu ya hii siku zitarudi mujarabu kabisa!

Zinedine Zidane, dunia ikiwa inamtambua kama mchezaji bora kabisa tena aliyepata fursa ya kutunukiwa tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa dunia mara tatu, yani mwaka 1998, 2000 na 2003. Siku hiyo alijikuta akifanya kitu cha ajabu na cha fedheha kubwa katika mchezo wa soka kwa kumtundika kichwa cha kifuani mlinzi wa timu ya taifa ya Italia Marco Materazzi baada ya kutokea vita ya maneno baina yao.

Sio watazamaji tu walioshtushwa na kitendo kile, hata mwalimu wa kikosi cha Ufaransa wakati huo Raymond Domenech na benchi lake la ufundi hawakuamini sio tu kutokea kwa tukio hilo, lakini pia kufanywa na ‘Zizzou’ tena akiwa nahodha wa kikosi chao. Zidane ni mchezaji aliyeheshimika sana katika ulimwengu wa soka, tukio la namna ile kutoka kwake halikutegemewa na yeyote yule.

Mwisho ule kwa Zidane ulikua wa kukarahisha sana, kuhitimisha safari yake ya kulitumikia taifa la Ufaransa kwa kutolewa nje ya uwanja kwa aibu ya adhabu ya kadi nyekundu sio kitu ambacho atakisahau kamwe. Na kingine kibaya ni kuwa matokeo ya kitendo kile yakaigharimu timu ikakosa ubingwa mbele ya Italia.

Zidane

Pamoja na kuwa mashabiki wa soka nchini Ufaransa walionesha kumsamehe na kumuunga mkono nguli huyo, sidhani kama yeye binafsi tayari amejisamehe kwa maamuzi yale. Pengine Zizzou angemaliza dakika zile za mwisho mwisho angefanikiwa kufanya jambo na kufanya mechi ile isifike hatua ya ‘matuta’,  lakini hayo yamekwishapita. Historia imeshaandikwa na hakuna anaeweza kuibadili.

Zidane amewahi kunukuliwa mara kadhaa na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa anaumizwa na tukio lile, lakini mara zote hizo amekataa kumuomba msamaha Materazzi. Alikwishawaomba msamaha wachezaji wenzake wa Ufaransa, mashabiki na ulimwengu mzima wa soka kwa kile kilichotokea.  Lakini kuliko kumuomba msamaha Materazzi ni bora afe!

Inasemekana kuwa Materazzi alimtukania Zidane mama yake na ndiyo sababu Zizzou alipatwa na hasira hali iliyopeleka kufanya tukio lile, lakini yeye Materazzi alisema kuwa hakumtukania mama bali dada yake. Kwa hiyo jambo moja liko bayana, Materazzi alimtusi Zidane. Kipo kitu alichokua anakitafuta kwa Zizzou, na bila shaka alikipata kwani kichwa kile kilitua vyema kabisa mwilini mwake na maumivu aliyoyapata hatokuja kuyasahau. Walisema waswahili, mwana kuyataka mwana kuyapata.

44 Komentara

    Mnatujuza mengi #meridian bet

    Jibu

    Zidane ni mchezaji niliekuwa na mkubalia sana

    Jibu

    Asanteeee meridian kwa taarifa

    Jibu

    Asanteh kwa taarifa meridian tunawapat vizur

    Jibu

    Hii ndosi itakumbukwa milele

    Jibu

    Asante meridianbet kwa kutupatia taarifa

    Jibu

    Mnatupatia wateja wenu kile tunachostahili

    Jibu

    Asnte kwa taarifa meridian mko juu..

    Jibu

    pale mzee mzima zizu alikua na jazba akakosa hata uchezaji bora, maana alilimwa kadi nyekundu ikionesha utovu wa nidhamu. ila meridian kwa kuchimbua mambo hata hili?

    Jibu

    Meridian mnatupatia kweli asnten sana

    Jibu

    Naikumbuka hii gemu ilinitoa machozi

    Jibu

    Kumtusi mtu si Jambo zuri na mtu anapokuwa amefanyiwa hivyo yuko radhi kutanya chochote kuridhisha nafsi yake kwa hy zidane alikuwa sahihi kufanya vile ili kupunguza Asira alizokuwa nazo.

    Jibu

    Asante kwa taarifa kama hii

    Jibu

    zidane alikuwa mtata hukiingia kweny anga zake

    Jibu

    Nakumbuka hii gemu iliniuma sana

    Jibu

    Mimi nilikuwa siyajui yote haya lakini baada ya kujiunga na app ya meridianbet ,sipitwi na habari yoyote.

    Jibu

    Habar hii ni nzur sana kwetu mashabik axanten

    Jibu

    Kwelii aise mwana kuyataka mwana kuyapata

    Jibu

    zidane mtu mbaya

    Jibu

    hasira hasara utakiw kuruhusu hasira ikutawale

    Jibu

    Zidane alikuwa ataki masihara alikuwa Atari sana uyo

    Jibu

    Asanten sana kwa taarifa meridianbet

    Jibu

    kwakweli zzizou alitia huruma

    Jibu

    Mtoto akililia wembe muache umkate

    Jibu

    Asantee kwa taarifa nzuri

    Jibu

    Zizzou pale alizinguwah kwl hakutumiah busara za kiutuuzima wake na hta burudan ya michezo ilipunguwah kiasi fulan Asante meridian kwa habar za kisport

    Jibu

    ahsanteni meridian bet kwa taarifa njema

    Jibu

    Zidane akaona aachane kabisa na soka baada ya hyo game

    Jibu

    Asante kwa kutujuza

    Jibu

    Mko vizuri na huduma zenu

    Jibu

    Mnatisha Sana jamanii

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Mpira una mambo mengi sana, lakini hapa Zidane kuwa alipitia kucheza mpira wa chandimu.

    Jibu

    Zidane akufanya kitendo Cha kinizam

    Jibu

    Nakumbuka fundi zizzou alifanya yake.
    Mwoshi wa siku akalimwa red Card najua zilikuwa figisu za materazi.

    Jibu

    Asante kwa taarifa meridianbet

    Jibu

    Kupewa nyekundu kwa Zizou kuliikosesha France ubingwa kwa asilimia Fulani

    Jibu

    Asantee meridian kwa taarifa

    Jibu

    Kwakwel meridian mnanipa habari nzuri sana tangu nijiunge na nyie kwakwl habari zote zinazohusiana na mpira nazipata kwenu nawapongeza kwa habari nzuri

    Jibu

    Icon zizzou

    Jibu

    Lilikuwa tukio la aibu sana. Asante kutukumbusha #meridianbettz

    Jibu

    Ahsante meridian kwa taarifa

    Jibu

    Mmh hilo sikichwa bali ndosi.

    Jibu

    Ulikuwa usiku wa kukumbukwa sana. Ni watu wachache hufikiria mara mbili kabla ya kutenda wanapopata hasira,ndio maana leo tujiuliza kwanini alifanya hivyo bila kufikiria dhamana aliyokuwa nayo!. Hata hivyo maisha yanatakiwa kuendelea. Asante kutukumbusha kisa hiki#meridianbettz

    Jibu

Acha ujumbe