Mchezaji wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uholanzi, Donny Van de Beek, amejikuta akiachwa kwenye orodha ya wachezaji 28 wa timu ya Uholanzi.
Kocha wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Louis Van Gaal ametoa orodha ya wachezaji watakaoipeperusha bendera ya nchi hiyo kwenye michezo miwili ya kimataifa mwezi ujao.
Hii ni mara ya pili kwa Van de Beek kuachwa kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya tukio hilo kutokea tena mapema mwezi huu kwenye michezo ya kimataifa. Sababu kubwa ya kuachwa kwa kiungo huyu, ni kutocheza kwa kiwango kinachotakiwa akiwa na Man United.
Donny ni miongoni mwa wachezaji wanaosugua benchi United akiwa amecheza mchezo 1 akitokea benchi (dhidi ya Newcastle United) na kuanza mchezo mmoja (dhidi ya Young Boys) ambapo pia hakucheza kwa dakika 90.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


