Villa Itambakiza Coutinho?

Licha ya kuwa amesajiliwa kwa mkopo, Philippe Coutinho anafanya mambo makubwa kule Aston Villa. Gerrard amelamba jokeri kwenye usajili huu.

Coutinho amejiunga na Villa kwa mkataba wa mkopo akitokea FC Barcelona ambapo, hakuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha klabu hiyo.

Ukiachilia mbali wakati mgumu aliokua nao kule Camp Nou, Coutinho wa Villa Park sio yule aliyekua anasugua benchi kule Catalunya. Hakika, “form is temporary but, classy is permanent” watoto wa mjini wanasema, “anaupiga mwingi!”

Villa

Steven Gerrard anafurahia uwepo wa Philippe kwa muda tu kwani, baada ya msimu huu anaweza kurejea Barca. Namna pekee ya kumbakiza kwenye kikosi chake, ni kumsajili moja kwa moja.

Katika hili, Steve G amethibitisha kuwa, uongozi wa klabu bado hawajaamua kuhusu Coutinho, wanamsajili moja kwa moja au watamuachia baada ya msimu?

Kitu cha muhimu kwa Gerrard ni kuhakikisha mchezaji huyo anakuwa kwenye mazingira mazuri na yanayomuwezesha kuonesha uwezo wake ambao wapenda soka wengi wanaujua toka alipokua Liverpool.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe