Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk alicheza mechi yake ya 60 ya Ligi ya Premia nyumbani bila kufungwa na kuweka rekodi mpya kwenye ligi kuu ya Uingereza.

 

Van dijk, Virgil van Dijk Aweka Rekodi Mpya Anfield., Meridianbet

Mholanzi huyo alicheza dakika zote 90 na kuondoka na alama 3 baada ya kumpa kichapo cha 1-0 West Ham United jana jioni.

Tangu ajiunge na Liverpool akitokea Southampton mwaka wa 2018, Van Dijk hajawahi kupoteza mchezo kwenye Premier League mbele ya mashabiki wa Anfield.

Kabla ya mchezo wa Jana, beki huyo wa kati alikuwa ameichezea Liverpool mechi 59 kwenye mashindano hayo, akishinda 51 na sare nane.

Hakuna mchezaji mwingine katika historia ya Premier League ambaye amefanikiwa kucheza mechi 60 za kwanza za Premier League nyumbani bila kupoteza.

Aliyeshikilia rekodi hapo awali alikuwa Lee Sharpe, ambaye aliichezea Manchester United misimu minne ya ligi tangu kuanza kwa shindano hilo mwaka 1992 bila kupoteza Old Trafford na kufikisha jumla ya mechi 59.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa