Mshambuiliaji wa kimatraifa wa Uholanzi Wout Weghorst ambaye anahusishwa na klabu ya Manchester United anatamani kujiunga na mashetani wekundu majira haya ya baridi.
Mshambuliaji Weghorst ambaye anakipiga klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki kwa mkopo kwasasa akitokea klabu ya Burnley ya nchini Uingereza. Mchezaji huyo ni mshambuliaji ambaye anafatiliwa kwa karibu na klabu ya Manchester dirisha hili dogo la Januari.Mshambuliaji huyo inaelezwa ana hamu ya kujiunga na Man United katika majira haya baridi huku akitambua kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag anaweza kumsajili moja kwa moja kama ataonesha ubora mkubwa ndani ya viunga vya Old Trafford.
Klabu ya Manchester United mpaka sasa ipo kwenye mazungumzo na vilabu vya Burnley na Besiktas kwajili ya kuhakikisha wanakamilkisha usajili wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi. Huku mchezaji mwenyewe akihitaji dili hilo likamilike haraka.Klabu ya Manchester United inahitaji kumsajili Wout Weghorst ili kuenda kuimarisha safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo inayoonekana kua na mapungufu, Mshambuliaji huyo anaonekana kua na gharama nafuu ambayo klabu hiyo inaweza kuifikia kwani klabu hiyo ilieleza mapema kua dirisha dogo hawatatumia pesa nyingi kufanya usajili.