Klabu ya Manchester United imefanikiwa kumalizana na mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi Wout Weghorst aliekua anakipiga klabu ya Besiktas kwa mkopo akitokea Burnley.
Manchester United ambayo iliweka wazi kua na kueleza mipango yake kwenye dirisha dogo la mwezi Januari ni kutafuta mshambuliaji atakayeweza kuimarisha safu yao ya ushambuliaji, Wout Weghorst ndio mshambuliaji aliekua amependekezwa na kocha wa timu hiyo Erik Ten Hag.Manchester United imefanikiwa kumpata mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi akitokea klabu ya Besiktas kwa mkopo akitokea klabu ya Burnley ilioshuka daraja msimu uliomalizika, Klabu ya Man United imefanikiwa kulipa kiasi cha paundi ya milioni 3 kwa klabu ya Besiktas.
Wout Weghorst anakwenda klabu ya Manchester United kuimarisha safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo ambayo inaongozwa na Marcus Rashford, Martial, pamoja Antony. Man United ilihitaji mshambuliaji halisia na ndio sababu ya kumsajili mchezaji huyo.Mshambuliaji Wout Weghorst anatarajiwa kusafiri kutoka nchini Uturuki kuelekea jiji la Manchester kwajili ya kufanya vipimo vya afya na kusaini mkataba kamili kwajili ya kuanza kuitumikia klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu.