Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi amekubali kuwa kibarua chake kwenye klabu ya Barcelona kiko hatarini kama hatafanikiwa kuiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wowote msimu huu.
Ijapokuwa Xavi alionesha matumaini makubwa tangu achukue mikoba ya Ronald Koeman mwezi Novemba, Lakini mambo yamenza kumuenda mrama baada kuondolewa kwenye michuano ya kombe la ulaya.
Licha ya kutumia kiasi kikubwa kwe dirisha la usajiri kipibdi cha majira ya kiangazi lakini bado alishinda kufurukuta kwenye mashindani ya ulaya baada ya kupoteza kwa Bayern Munich na kutoa sare na Inter Milan kwenye hatua ya makundi.
Xavi aliwaambia waandishi: “Ndio hiyo haibadili, narudia hili. Malengu, ya kikosi na wachezaji hawa ni kushinda ubingwa. Tunapaswa kushinda ubingwa.
“Nadhani tunapaswa kujenga timu itayoweza kushinda ubingwa, bado nina shauku kwenye hii dunia, licha ya kwamba nimekuwa nikikosolewa sana hii wiki. Kila mtu amekuwa akinipa moyo, simu yangu ya mkono imukuwa busy kutumiwa text kama vile kuna ndugu yangu amefariki.
Ikiwa nitashinda hili, kutakuwa na matokeo yake, lakini kwa sasa nimekuwa mtulivu. Nadhani tunakikosi cha kuweza kushinda ubingwa, kama hatuta shinda ubingwa, kocha mwingine atakuja kujaribu pia.”