Moja ya wachezaji bora wa ligi ya kikapu nchini Marekani NBA Klay Thompson anayeichezea klabu ya Golden State Warriors ameweka wazi kuwa siri ya mafanikio ya timu hiyo ni kocha wao Steve Kerr kwa kuwapa hamasa ya ushindi.
Golden State Warriors wamekuwa wakisherekea msimu wao bora wa nne kwenye ligi ya NBA ndani ya misimu nane iliyopita huku wakiibuka na ushindi safi wa kuvutia dhidi ya Los Angeles Lakers.
Baada ya ushindi wa usikuwa kuamkia jumatano, Thompson aliulizwa kuhusu mijongeo ya mpira na alimtaja kocha wao kuwa yeye ndiye aliyenazisha mfumo huo wa uchezaji, alisema: “Nitoe heshima kwa Steve Kerr, yeye alikuja na maono na kuchochea moto huu.
“Steve Kerr alitupa mfano thabiti, Klabu ya FC Barcelona na mchezo wao tiki taka, ni mchezo wa pasi za kufungua kwa mtu aliyekuwa na nafasi.
“Na sisi, tunatoa pasi kwa mtu aliyechukua nafasi, huku ukizidi kusogea na kucheza na kupokea tena pasi na uwezo wa Steoph vile vile Draymond. Kwa sababu anaweza kurahisisha, sawa na Andrew Wiggins na Jordan Poole.”