Zlatan Nje AC Milan Dhidi ya Juventus

Zlatan Ibrahimovic na Olivier Giroud hawajajumuishwa kwenye orodha ya kikosi cha AC Milan kwa ajili mechi ya leo dhidi ya Juventus, wakati Mike Maignan akirejea.

Kwa mujibu wa La Gazzetta dello Sport, kipa huyo wa Ufaransa hayuko fiti kabisa baada ya changamoto ya jeraha la mkono wake.

Mlinda mlango huyo wa zamani wa Lille alipata jeraha kidogo wakati wa mechi ya AC Milan dhidi ya Liverpool pale Anfield mapema wiki hii, lakini amejumuishwa kwenye kikosi kinachosafiri kwenda Turin.

Tiemoue Bakayoko, Rade Krunic na Davide Calabria pia hawapo kikosini kwa sababu ya majeraha.

Ante Rebic atakuwa mshambuliaji pekee wa Milan kwenye Uwanja wa Allianz usiku wa leo na Alexis Saelemaekers, Brahim Diaz na Rafael Leao wakiwa nyuma yake.

Andrea Conti pia anaungana na kikosi huko Turin licha ya kutokuwa sehemu ya mipango ya Pioli msimu huu. Beki wa kulia wa Italia alitumia sehemu ya pili msimu wa 2020-21 kwa mkopo huko Parma.

AC MILAN SAQUAD without Zlatan

Kikosi cha AC Milan dhidi ya Juventus

Golikipa: Jungdal, Maignan, Tatarusanu

Walinzi: Ballo-Touré, Conti, Florenzi, Gabbia, Hernandez, Kalulu, Kjaer, Romagnoli, Tomori

Viungo: Bennacer, Castillejo, Diaz, Kessie, Saelemaekers, Tonali

Washambuliaji: Leao, Maldini, Pellegri, Rebic


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.