Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa ulaya ‘Uefa’ huku kocha wa klabu hiyo akipata heshima ya kuiwezesha klabu hiyo kuchukua ubingwa 14 wa ulaya msimu uliopita.

Karim Benzema alikuwa na kiwango bora na kufanikiwa kufunga magoli 15 kwenye mashindano hayo, na kuiongoza timu hiyo kuifunga Liverpool kwenye mchezo wa fainali nchini Ufaransa.

Karim Benzema

Benzema alifanikiwa kufunga hat-tricks kwenye michezo dhidi ya PSG na Chelsea, na pia akifunga mara tatu kwenye hatua ya mtoano wa nusu fainali mbili dhidi ya Manchester City.

Real madrid pia walifanikiwa kushinda ubingwa wao wa 35 wa La liga, huku wakifanikiwa kumaliza kwa pointi 13 zaidi ya wapinzani wao Barcelona, na Karim Benzema akimaliza kama mfungaji bora wa ligi hiyo akifunga magoli 27 na akimaliza na jumla ya magoli 44 kwenye michezo ya mashindano yote.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa