Costa Rica Wafufukia kwa Japan

Timu ya taifa ya Costa Rica imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza kwenye mochuano ya kombe la dunia mwaka huu baada ya kuifunga timu ya taifa ya Japan mapema leo.

Timu hiyo chini ya kocha Luis Fernando Suarez imefanikiwa kupata alama tatu baada ya kushinda bao moja kwa bila dhidi ya Japan katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi E. Goli la Keysher Fuller Spence dakika ya 81 ya mchezo lilitosha kabisa kuipatia timu hiyo alama tatu muhimu.costa ricaCosta Rica ambayo ilikua ndio timu iliyofungwa magoli mengi kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu lakini imeweza kuinuka na kuweza kupata alama tatu leo dhidi ya Japan ambayo mchezo wa kwanza ilifanikiwa kuifunga timu ya taifa ya ujerumani.

Baada ya matokeo ya Costa Rica leo imeendelea kulifanya kundi hilo kua gumu kwani mpaka sasa timu tatu zina alama tatu huku ni Ujerumani tu ambao hawapata matokeo ya ushindi huku wakiwa na kibarua kizito usiku wa leo dhidi ya Hispania.

costa ricaMchezo wa Hispania dhidi ya Ujerumani utatoa taswira halisi ya kundi hilo kwani Ujerumani akishinda mchezo wa leo usiku dhidi ya Hispania ina maana kundi hilo kila timu itakua na alama tatu na kundi litakua wazi mpaka mchezo wa mwisho ndio utaliamua kundi hilo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.