Kocha mshahuri na aliyewai kuvifundisha vilabu vikubwa barani Afrika Pitso Mosimane leo ametoa shukrani zake kwa klabu ya Yanga kwa kumwalika kwenye siku ya wananchi.

Pitso Mosimane ameshawai kufundisha timu ya taifa ya Afrika Kusini, Supersport United, Al Ahly na Mamelodi Sundowns. Pia Mosimane amefanikiwa kuchukua ubingwa wa Afrika mara tatu akiwa na klabu mbili, huku akiweka rekodi bora akiwa na Al Ahly ambapo alifanikiwa kuchukua ubingwa wa afrika mara mbili mfululizo.

Pitso Mosimane, Pitso Mosimane Aishukuru Yanga kwa Mwaliko, Meridianbet

‘Safari ya Yanga kwenye siku ya wiki ya mwananchi itakuwa moja ya kumbukumbu kwenye kitabu changu. Sitakuja kuisahau hii wiki na utamaduni wa soka la Tanzania umenivutia sana.

“Kwa raisi, rafiki yangu Eng Hersi, asante sana kwa mwaliko. Nina bahati kwamba mwaliko ulikuwa wakati sahihi. Endelea kufanya kazi yako bora kwenye soka ndani ya jamii yako, hakika unafanya mabadiliko.

‘GSM, wafanyakazi, wachezaji na mashabiki wa Yanga, asante kwa ukaribisho na kunifanya nijisikie niko nyumbani, kiukweli niliufurahia muda wangu. Hadi tutakapokutaba tena.” Aliandika Pitso Mosimane kwenye ukarasa wake wa twitter.

Pitso ndio kocha wa kwanza ambaye siyo raia wa nchi Misri na mweusi kufundisha klabu ya Al Ahly.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa