David de Gea ambaye ni mlinda mlango wa Manchester United, ameibuka mtandaoni kwa kuchapisha picha yenye ujumbe maalum “dedication” kwa bibi yake, hiyo ni baada ya ushindi wa jana wa Man utd waliokuwa ugenini dhidi ya Leicester wa goli 0-1.

De Gea, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter na Instagram kuwa uwezo wake wa kuokoa mpira wa adhabu usiingie golini kwake pamoja na ushindi wa jana, ni zawadi kwa bibi yake kipenzi popote alipo.
View this post on Instagram
View this post on Instagram
Mbali na kipa huyo, pia wachezaji wengine wa timu hiyo waliposti jumbe mbalimbali kuelezea hisia zao kwa matokeo ya jana ambapo nahodha wa timu hiyo ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ureno Bruno Fernandes aliandika kuwa anawashukuru mashabiki kuwa pamoja na wao, hivyo wajiandae tena kwa mechi ya Jumapili dhidi ya Arsenal.


Hata hivyo staa wa kimataifa wa ureno Cristano Ronaldo, yeye hajaposti chochote kuhusiana na matokeo ya jana, huku posti yake ya mwisho kuhusu timu hiyo ni ile ya ushindi dhidi ya Southampton.


