ALIYEKUWA Mkurugenzi wa mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro ametambulishwa rasmi leo na uongozi wa Fountain Gate kuwa Mtendaji Mkuu.
Kandoro aliitumikia Yanga kwa muda mrefu ambapo aliondoka hivi karibuni ndani ya klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
Kupitia kurasa zao mbalimbali za mitandao ya kijamii Fountain Gate wamemtangaza Kandoro kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa taasisi hiyo.
“Thabit Kandoro amejiunga na Fountain Gate Academy Tanzania na kuwa Mtendaji Mkuu wa masuala yote ya michezo katika Taasisi.”

