UONGOZI wa klabu ya Yanga umefunguka kuwa tayari wageni wao Al Hilal wametuma barua kuwa wanatarajia kufika nchini kesho alhamis kwa ajili ya mchezo wao.

Yanga inapaswa kupata ushindi kwenye mchezo huo wa nyumbani ili kuhakikisha wanatinga katika hatua ya makundi kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Sudan.

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema: “Maandalizi yetu kama uongozi yamekamilika na hata yale ya nje ya uwanja.

“Ya nje ya uwanja ni kwa maana kwamba kuwaandalia wageni wetu sehemu ya kufikia kwani tayari wametuma taarifa kuwa wanatarajia kufika Dar kesho alhamis.

“Hatujaingia kwenye hatua ya makundi kwa muda mrefu hivyo mipango yetu ni kuhakikisha tunaiweka rekodi hiyo na wachezaji, benchi la ufundi wanalijua hilo na wameahidi kulitimiza.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa