KIKOSI cha Azam FC kinatarajia kuondoka Jijini Dar kesho alhamis kuelekea nchini Libya kwa usafiri maalum kwa ajili ya mchezo wao wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Akhdar.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Oktoba 8 mwaka huu nchini Libya katika kusaka nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Shirikisho barani Afrika.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka zakazi’ amesema kuwa: “Tuko vizuri na timu inatarajia kuondoka nchini kesho alhamis kuelekea nchini Libya tukiwa na usafiri binafsi.

“Kocha amependekeza kuondoka na jumla ya wachezaji 25 ambao wapo kwenye  mipango yake na hao wengine ni nafasi tu zimejaa na watatumika kwenye michezo mingine huko mbele.

“Wachezaji wawili tu ndio wenye majeraha ambao ni Keneth Muguna na Wilbol Maseke lakini kama watakuwa fiti mwalimu atawatumia kwenye michezo ijayo hivyo hawapo kwenye kikosi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa