MFADHILI wa zamani wa Simba Azim Dewji ambaye ni kaka wa mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ amewataka wachezaji wa Simba Kwenda Angola kwa tahadhari na wasitegemee kubebwa na historia.
Dewji alisema, wachezaji wanatakiwa kuhakikisha wanaheshimu kila dakika ya mchezo huo na wasiruhusu kufungwa ila wao wanatakiwa washinde angalau hata bao 1-0 au ikishindikana hata sare ila siyo kufungwa kabisa.

Akizungumzia mchezo huo Azim alisema: “Mambo ya kusema tunakwenda kuwafungwa kwao kirahisi inatakiwa tuyatoe kichwani. Wachezaji lazima wajue kuwa wana jukumu kubwa sana mbele yao.
“Hakuna historia kwenye soka, Simba siyo ya kucheza mashindano mengine zaidi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Wachezaji wasitegemee kuwa wakitolewa hapo watakwenda shirikisho. Simba inatakiwa Kwenda makundi na hadi nusu fainali.”
Simba wanatarajia kusafiri kesho kutwa Jumamosi Kwenda Angola kucheza mchezo wa kwanza na Premier Do Agosto ya Angola Oktoba 9 na wanatarajia kurudiana wiki mbili baadae hapa Dar es salaam.

