Moses Phiri Azua Mijadala

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Simba Moses Phiri amezua mijadala mbalimbali kwa kile kilichoonekana katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar na kumsababishia mchezaji huyo majeraha.

Mshambuliaji huyo ambaye aanaonekana kua hatari zaidi katika safu ya ushambuliaji ya Simba kwani akiwa amefunga mabao 10 mpaka sasa kwenye ligi kuu ya NBC, Amezua mijadala kwa wadau mbalimbali wa michezo kwa kudai mchezaji huyo anachezewa rafu mbaya na halindwi na waamuzi.moses phiriKatika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao ulipigwa katika dimba la Kaitaba Kagera Sugar dhidi ya Mnyama Simba na kumalizika kwa suluhu ya goli moja kwa moja, Ni dhahiri mchezaji huyo alikua anachezewa radu mbaya mpaka kupelekea kupata majeraha lakini mwamuzi wa mchezo hakuchukua hatua yeyote kitu kilichofanya wadau mbalimbali wa soka kukemea kitendo hicho.

Mshambuliaji huyo kwasasa amepata majeraha ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa muda ambao haujajulikana bado, Mchezaji huyo ameonekana kuposti picha kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akiwa na magongo kuashiria amepata majeraha.moses phiriTaarifa ya kuumia kwa Moses Phiri imekua sio taarifa njema kwa mashabiki wa klabu ya Simba, Kwani mshambuliaji huyo ndio amekua akionekana msaada mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu ya Simba kwasasa.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.