Kiungo mpya wa klabu ya Real Madrid ambaye amejiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Borussia Dortmund Jude Bellingham amesema hajajiunga na klabu hiyo kwasababu ya pesa.
Kiungo Bellingham amesema hayo wakati wa utambulisho wake rasmi leo akisema kua kujiunga na klabu ya Real Madrid haikua suala la pesa kwani klabu hiyo ni klabu kubwa kabisa ulimwenguni na ndio sababu ya kiungo kujiunga na wababe hao wa soka duniani.
Kiungo huyo ameweka wazi kua sababu kubwa iliyomfanya kujiunga na klabu ya Real Madrid ni pale alipohudhuria mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kati ya Real Madrid dhidi ya Liverpool ambapo Real walishinda kwa bao moja kwa bila na ndipo alipoona kujiunga na Madrid ni uamuzi sahihi kwake.
Jude Bellingham amejiunga na klabu ya Real Madrid kama mchezaji ghali kabisa msimu huu kwenye kikosi cha klabu hiyo na kwake amesema kujiunga na klabu hiyo ni kama ndoto kutimia kwake kwani klabu hiyo ni ndoto ya wachezaji wengi duniani.
Kiungo Bellingham atavaa jezi namba tano ambayo ni jezi yenye heshima sana klabuni hapo kwani imevaliwa na magwiji mbalimbali na mmoja wao ni Zinedine Zidane ambaye kwa Jude ni kama kioo kwake na wengi wanaamini mchezaji huyo ataitendea haki jezi hiyo.

