Klabu ya Real Madrid CF imepigwa faini ya euro 15,000 na UEFA baada ya shabiki mmoja kuonekana akifanya ishara ya Nazi wakati wa mchezo wa marudiano wa hatua ya mchujo ya UEFA Champions League dhidi ya S.L. Benfica uliochezwa wiki iliyopita.

UEFA ilithibitisha adhabu hiyo leo Ijumaa, ikieleza kuwa kitendo hicho kilionekana wakati wa matangazo ya moja kwa moja ya mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Santiago Bernabéu Stadium jijini Madrid.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Baada ya tukio hilo, Real Madrid ilitoa taarifa ikisema kuwa mara moja waliagiza kamati ya nidhamu ya klabu kuanza taratibu za kumfukuza mwanachama huyo aliyerekodiwa akifanya ishara hiyo inayokatazwa.

Klabu hiyo ilieleza kuwa mtu huyo alitambuliwa na walinzi wa usalama wa uwanjani muda mfupi baada ya kuonekana kwenye matangazo ya televisheni na aliondolewa mara moja ndani ya uwanja huo huku klabu ikilaani vikali kitendo hicho.

Mbali na faini hiyo, UEFA pia imeiamuru Real Madrid kufunga sehemu ya viti 500 vilivyopo katika jukwaa la chini la upande wa kusini wa uwanja huo kwa mchezo mmoja wa mashindano ya Ulaya, ingawa adhabu hiyo imesimamishwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Katika mchezo huo, Real Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Benfica na kufuzu hatua ya 16 bora kwa jumla ya mabao 3-1, ambapo sasa itakutana na Manchester City F.C. katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.


