Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) limethibitisha kuwa litakata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kufuatia kunyang’anywa ubingwa wa Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 katika uamuzi waliouita “usio wa haki na usiokubalika.”
Uamuzi huo umetolewa na Bodi ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambayo ilibatilisha ushindi wa Senegal wa mabao 1-0 dhidi ya wenyeji Morocco na badala yake kuipa Morocco ushindi wa mabao 3-0. FSF imesema hatua hiyo inaharibu heshima na uaminifu wa soka barani Afrika.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa mujibu wa CAF, Senegal ilikiuka kanuni za mashindano baada ya baadhi ya wachezaji wake kutoka nje ya uwanja kwa muda wakipinga penalti iliyotolewa dakika za mwisho kwa Morocco, hali ambayo ilitafsiriwa kama kuikimbia mechi kwa mujibu wa vifungu vya 82 na 84 vya kanuni za AFCON.
Hata hivyo, Senegal wanapinga vikali uamuzi huo wakisisitiza kuwa ni mwamuzi pekee wa uwanjani ndiye mwenye mamlaka ya kuamua hatma ya mchezo, na hawakubaliani na kubadilishwa kwa matokeo baada ya mechi kumalizika.
Katibu Mkuu wa FSF, Abdoulaye Seydou Sow, amesema hawatakubali uamuzi huo na tayari wanaandaa hatua za kisheria kwenda CAS, akisisitiza kuwa wako tayari kupigania haki ya soka la Senegal hadi mwisho.
Kwa upande wao, Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) limesema linaunga mkono uamuzi huo likieleza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha kanuni za mashindano zinafuatwa kikamilifu na kulinda utulivu wa soka la Afrika.

