CAS Yapokea Rufaa Ya Senegal Kupinga Uamuzi wa CAF

Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo, CAS, imethibitisha rasmi kupokea rufaa kutoka Shirikisho la Soka Senegal (FSF) kupinga uamuzi wa CAF wa kuwanyang’anya ubingwa na kuikabidhi Morocco.

CAS Yapokea Rufaa Ya Senegal Kupinga Uamuzi wa CAFKupitia taarifa yake, Katibu Mkuu wa CAS, Matthieu Reeb, amewahakikishia wadau wa soka kuwa mchakato huo utashughulikiwa kwa haraka huku ukizingatia haki kwa pande zote zinazohusika.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

“Tumejipanga kikamilifu kushughulikia kesi hii, na tutahakikisha mchakato unaenda kwa kasi iwezekanavyo bila kuathiri misingi ya haki,” alisema Reeb akizungumzia uzito wa shauri hilo.

CAS Yapokea Rufaa Ya Senegal Kupinga Uamuzi wa CAFSenegal waliibuka na ushindi wa mabao 1-0 katika fainali iliyochezwa mwezi Januari, lakini baadaye CAF ilibadili matokeo hayo na kuipa ushindi Morocco kwa mabao 3-0 kwa njia ya ‘forfeit’.

Uamuzi huo wa CAF ulitokana na tukio la wachezaji wa Senegal kugoma na kutoka nje ya uwanja kwa muda wakipinga penalti iliyotolewa kwa upande wa Morocco, jambo lililotafsiriwa kama ukiukwaji wa kanuni za mchezo.

CAS Yapokea Rufaa Ya Senegal Kupinga Uamuzi wa CAFSasa macho na masikio ya wadau wa soka yanaelekezwa CAS, ambayo inatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho utakaoamua kama kombe hilo litarudi Dakar au litaendelea kubaki Rabat.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.