Katika soka mashabiki wamekuwa na nguvu sana katika kushinikiza baadhi ya maamuzi ya timu. Mashabiki huungana na wachezaji, kwa nafasi yao huwa wanakuwa na shinikizo lenye nguvu sana kwenye mamlaka za juu za vilabu kufanya maamuzi magumu. Hebu tuone kwa Chelsea mgomo unaweza kuwa na athari gani?
Mamia ya wamiliki wa tiketi za msimu za Chelsea wametangaza kuuza siti zao kwenye gemu zinazofuata za Ligi Kuu ya Uingereza za klabu hiyo ikiripotiwa kuwa huo ni mgomo dhidi ya meneja Maurizio Sarri.
Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, zaidi ya watu 400 wamejiorodhesha kuuza siti zao kwenye debi inayokuja dhidi ya West Ham United Aprili 8. Waklati huo, Mashabiki wengine wanaokaribia 700 pia wameweka tiketi zao sokoni za gemu dhidi ya Burnley Aprili 22. Inadaiwa kuwa mashabiki hawajapanga kuhudhuria gemu hizi.
Hata hivyo, inaaminika kuwa maneno maneno juu na ishara zote za mgomo zinazoendelea zinaweza kuwasukuma zaidi uongozi wa juu wa klabu hiyo kufanya maamuzi ya kumtimua Maurizio Sarri ambaye pia amewahi kuwa meneja wa Napoli. Ripoti zinadai kuwa mashabiki hawapendezwi na aina ya mpira aliyoishikilia meneja huyo, maarufu kama ‘Sarri Ball’
Cheslea kwa sasa wana pointi 3 nyuma kuikuta nafasi ya 4 ili waweze kushiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao, pia wapo kwenye robo fainali ya Ligi ya Europa.


Issa
Aondoke tu sarri
Furahav
Hatari