Mabingwa wa La Liga, Barcelona wanaripotiwa kuwa wapo kwenye mishe mishe za kutaka kuwasajili mastaa wa Manchester United kutoka Ligi Kuu ya Uingereza. Ripoti zinadai kuwa Barca wameshaanza kufanya mawasiliano ya kujua nani ataingia klabuni hapo.
Mastaa wa Man United, Juan Mata na Marcus Rashford wamekuwa wakihusishwa na klabu ya Barcelona tokea Ole Gunnar alipochukua nafasi ya Jose Mourinho mwezi disemba.
Hata hivyo, wakati taarifa zikibainisha kuwa Barca tayari wameanza taratibu za kuwanasa mastaa pale United, Rashford anatajwa kutokuwa miungoni mwa wachezaji ambao klabu ya Man Utd watawapoteza.
Taarifa za hivi karibuni zinadai kuwa Barcelona wanahitaji kupata mbadala wa kudumu wa Luiz Suarez huku Juan Mata akiwa kipaumbele choa kwa sasa. Mata atakuwa mchezaji huru msimu huu wa joto akiwa bado anafikiria kama anahitaji kuongeza mda mwingine klabuni United.
Kwa mujibu wa The Sun, Barcelona wamewasiliana na baba pia wakala wa mchezaji huyu kuangalia uwezekana wa staa huyu mwenye miaka 30 kurejea nyumani.


aisha
Barcelona waangalie maamuzi yao
Povel
Habar njema
Issa
Wawachukue tu united kuna vipaji kibao