Sakata la Paul Pogba kuhusishwa na Real Madrid linaendelea kuwa tamu zaidi! Ipo wazi kuwa Pogba anatamani siku moja kuichezea klabu ya Real, na alinukuliwa akijihusisha na klabu hiyo siku kadhaa zilizopita. Zinedine zidane naye hajapepesa macho wala maneno kusema jinsi anavyomezea mate Pogba na uwezekano wa kumchukua.
Zidane ana wiki kadhaa tu toka aliporejea klabuni Real kama meneja akitarajia kufanya makubwa klabuni hapo. Baada ya sakata zima la Pogba kuhusishwa na klabu8 ya Real Madrid ambayo kwa sasa inasaka kujiboresha zaidi kwa kusajili wachezaji bora, Zidane amesema kuwa na yeye pia ana mkubali nyota huyu wa Manchester United na angependa nyota huyu aingie Real Madrid siku moja.
“Nampenda sana, sio kitu kigeni. Ninamfahamu yeye binafsi. Kiukweli ni mchezaji wa tofauti kabisa, wachezaji wachache sana wanaweza kufanya kile anachoweza kufanya. Ni kiungo anayeweza kulinda, kushambulia, kufanya kila kitu.”
“Lakini siyo mchezaji wangu, ni wa Manchester. Amesema mara zote, ukiacha United, Madrid ndiyo sehemu inayomvutia. hivyo akimalizana na Manchester, kwa nini asije hapa Madrid? -Zinedine Zidane akimzungumzia Paul Pogba
Khadija
Duuh!!cjui itakuwaje#meridianbettz