Liverpool vs Tottenham, Dondoo za Gemu

Jumapili hii ni Liverpool vs Tottenham pale Anfield! Liverpool wanakutana na kibarua kingine kigumu wanapomkaribisha Tottenham Hotspur, kikwazo ambacho kinaweza kuwaonesha muelekeo wa kutwaa ubingwa au kupigwa gepu zaidi na Manchester City.

Liverpool wapo chini ya Machester City kwa pointi 1, wanahitaji kushinda gemu ya hii ili waweze kurejea kileleni wakati ambao Manchester City ana akiba ya gemu moja mezani zaidi yao.

Gemu dhidi ya Spurs ni gemu muhimu kwao kupata pointi 3 kuendelea kuwa karibu zaidi na ubingwa, wasipokaa sawa wanaweza wakajikuta wamesalia tu nafasi ya pili.

Liverpool

Liverpool wana rekodi nzuri nyumbani. Mpaka sasa wana rekodi ya gemu 36 bila kuchapwa wakiwa nyumbani, wanahitaji mno pointi hizi ili waendelee kuwa katika nafasi nzuri.
Gemu zao za mwisho wameshinda gemu 4 na sare 2 katika gemu 6 za EPL. Katika gemu 6 za michuano yote wameshinda 4 na sare 2 pia.

Tottenham Hotspur
Baada ya Ushindi dhidi ya Leicester hawajaweza kukusanya pointi zote 3 katika gemu zao 4 zilizofuata wakiambulia kichapo kwenye gemu 3 na kutoa sare gemu 1.

Spurs wana afadhari ya pointi moja dhidi ua Arsenal katika nafasi ya 3 ambayo wameikalia, wanahitaji ushindi wajiweke mbali zaidi na Arsenal ambao pia wana hatari ya kupinduliwa na United. Hii inafanya Liverpool vs Tottenham Jumapili kuwa mchezo mgumu zaidi.

Vikosi vinavyotarajiwa

Liverpool: Alisson; Alexander-Arnold, Matip, Van Dijk, Robertson; Henderson, Fabinho, Wijnaldum; Salah, Firmino, Mane

Tottenham Hotspur: Lloris; Trippier, Alderweireld, Vertonghen, Rose; Sissoko, Wanyama, Eriksen; Dele; Son, Kane

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.