Hatma ya Gareth Bale pale Real Madrid inaonekana kuwa kama giza lisiloeleweka mwisho wake. Gareth Bale amekuewa katika kipindi kigumu akishindwa kuwa katika fomu nzuri kama wanavyomtarajia. Zidane ataamua hatama yake mwisho wa msimu huu.
Staa huyu alijikuta ameshindwa kumpendeza sana Santiago Solari kwa kipindi cha hivi karibuni huku uhusiano wake na Zidane wakati yupo klabuni hapo ukidaiwa kuwa ulikuwa wa mashaka. Ikumbukwe kuwa Zidane anadaiwa kuwa yeye alipendelea staa huyu ndiye angeuzwa badala ya Cristiano Ronaldo.
Hata hivyo, Zidane na Bale wanaripotiwa kuwa wanatofautiana katika staili ya mchezo ambayo Bale anacheza, lakini aliweza kumuacha kwenye kikosi cha kwanza katika gemu yake ya kwanza aliporejea Real Madrid dhidi ya Celta Vigo.
Zidane anasema kuwa baada ya kumaliza gemu zilizobakia basi wataona nini kinapaswa kifanyike, hata hivyo anamuona Bale kama mchezaji muhimu na mwenye mchango chanya kwa klabu na amefanya mambo mengi tayari. Anaamini Bale anajituma, na anafurahia kuwa klabuni hapo. Bila shaka Bale anaweza kuamua pia hatma akiwa anahusishwa na klabu kadhaa.


aisha
good news
Povel
Bale fundiiiii
Frank Patrick
hizi taarifa zinakuwa na sintofahamu sana mara zidane hamtaki lkn tunaona anamtumiaga
Fatina mfingi
Bale jembe