Lionel Messi ni mchezaji ambaye anaogopwa sana kwenye Ligi ya Uhispania na Ulaya kwa ujumla wake. Anafahamika vyema kwa kupindua matokeo. Bila shaka huyu anweza kuwa mwiba na kuwaletea balaa Man United katika kuwania nafasi ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Andy Cole amewaonya klabu yake ya zamani ya manchester United kuwa Messi anaweza kuwa mwiba kwa maajabu ambayo anaweza kuyafanya klabuni hapo, bila shaka maandalizi ya United yatakuwa yanazindatia namna ya kumzuia staa huyu lakini mara kadhaa amekuwa akicheka na nyavu kwa mazingira ambayo siyo rahisi kwa nyota mwingine kupenya.
Cole anaamini Barcelona wanategemea kwa kiasi fulani maajabu ya staa huyu ambaye akiamua kufanya mambo anafanya kweli!
Watabe hawa wa La Liga, Barcelona wanatajwa kuwa na nafasi nzuri ya kuibuka mabingwa lakini imani ya Solskjaer na mashabiki wengi wa United wanaamini wanaweza kuwaletea muskheri mabwana hawa na kuinasa nafasi ligi ya nusu fainali ila balaa la Messi ni changamoto.
United wanakumbuka walipokuwa mabingwa mwaka 1999 walipocheza na Barcelona gemu zote mbili zikaisha kwa sare 3-3, kila timu ikiwa na aina yake ya ushambuliaji. Cole anaamini United wakiamua kucheza kama wanavyofanya wakati wote wanaweza kuondoka na matokeo mazuri.



Issa
Mess hafai kabisa