Klabu za PSG, Manchester United na Juventus zinaripotiwa kuongoza mbio za kumnasa staa wa Lyon anayecheza nafasi ya kiungo Tanguy Ndombele.
Staa huyu mwenye miaka 22 ambaye amekwishacheza mara 4 kwenye kikosi cha taifa cha Ufaransa amewavutia Juventus kwa mda sasa, Juve wanaonekana bado hawapo tayari kuacha kumfukuzia.
Lyon wao walimnunua kutoka AMiens kwa paundi milioni 8 tu, lakini raisi wa klabu hiyo anatarajia kupokea kati ya paundi milioni 70-80 kwa staa huyo.
Kwa mujibu wa Jarida la ufaransa, L’Equipe, Juve wapo kwenye nafasi nzuri zaidi kumnasa wakifuatiwa na PSG na Manchester United.
Klabu hizi hazipo peke yake, mbio hizi zimeungwa tela na Liverpool, Chelsea na Manchester City. Wakati juhudi za kuinasa sahihi yake msimu ujao zikiendelea Chelsea wanamtaka nyota huyu kwa mkopo.


Ernest
Tanguy Ndombele. mwamba sasa anakipika Spurs
Povel tz
Ndombele yupo vzr sana