Safari ya matumaini ya Manchester United kumaliza kwenye ligi wakiwa nafasi 4 za juu imeingia doa leo baada ya kupata kichapo dhidi ya Everton. De Gea anakuwa golikipa wa kwanza wa EPL kufungwa magoli mengi ya nje ya boksi.
Mashetani Wekundu wameshindwa kufurukuta kwenye kuta za Godison Park na kukubali kichapo cha bao 4-0. Kuelekea gemu hii United walikuwa nafasi ya 6, na kama wangeshinda mechi hii basi wangewapiku wapinzani wao Chelsea na kuwa na nafasi nzuri zaidi kupambania 4 bora.
De Gea Kuchapwa Magoli ya Mbali
De Gea ameruhusu magoli ya nje ya boksi tena, magoli ambayo ni nadra kufungwa kwa magolikipa wa aina yake. Huu ulikuwa ni wakati wa kuonesha ufundi binafsi kwenye gemu.
Kwa takwimu De Gea ndiye golikipa pekee aliyefungwa magoli mengi zaidi ya umbali mrefu kwenye ligi ya EPL. Amefungwa jumla ya magoli 5 kutoka nje ya boksi. Mkwaju wa Sigurdsson uliobamba nyavu ulikamilisha idadi ya magoli 4 ya mbali aliyofungwa nyota huyu. Shambulizi la Digne kutoka mbali pia lilimtia wenge De Gea kukamilisha idadi ya 5.
Everton wameweza kuwatawala vyema wageni wao ambao na kutumia vyema udhaifu wa safu ya ulinzi ya Man United kujipatia faida ya magoli 4. Kwa gemu zilizobaki nafasi ya Manchester United kumaliza kwenye 4 bora imezidi kuwa nyembamba mno, anahitaji kuwaombea wapinzani wake wapoteze gemu zilizo mbele yao na yeye ashinde alizobakia nazo ambazo ni ngumu zaidi ya gemu aliyocheza leo.


Furahav
De Gear anajua.