Anthony Joshua anatarajia kuwa na pambano lake la kwanza kabisa nchini Marekani mwezi June, staa huyu alikuwa amepangiwa kupambana na Jarrell Miller kwenye pambano hilo pale Madison Square Garden. Luis Ortiz alitarajiwa kuwa mbadala wa Miller.
Miller alinyimwa kibali na baada kugundulika kama alijihusisha na matumizi yasiyo sahihi ya madawa. Luis Ortiz, mpiganaji kutoka Urusi amechomoa ofa ya kupambana na bingwa huyu kutoka Uingereza, King Kong Boxing wanaisisitiza kuwa promota wa wa Anthony Joshua anamtumia Ortiz kwa ajili ya kiki.
King Kong Boxing wanasema ofa kama ile haiwezi kupokelewa kwao na hawawezi kushiriki kwenye kwenye dili hili la June.
Mpinzani mpya wa Anthony Joshua anatarajiwa kutangazwa wiki hii huku Joshua akiendelea na maandalizi ya pambano. Wapiganaji 8 wanatajwa kuwa kwenye orodha ya wanaoweza kuwa mbadala wa Miller, wanaoangazia sana walikuwa ni pamoja na Ortiz, Adam Kownacki and Michael Hunter.


Furahav
Michezo ya ngumi huwa naipenda sana.
Povel
Habar njema