Aliyekuwa meneja wa Brighton Hove Albion, Chris Hughton ameamua kufunguka ikiwa ni siku chache baada ya kutimuliwa na klabu hiyo. Meneja huyu a zamani wa klabu hii amesema kuwa kutimuliwa kwake kulikuwa ni kitu ambacho hakukitarajia kabisa na kimemvunja moyo.
Chris ambaye ana umri wa miaka 60 aliisaidia klabu hii kufuzu kuingia ligi kuu ya Uingereza mwaka 2017. Alisepa klabuni hapo baada ya gemu ya mwisho kwa msimu huu kwenye ligi wakimaliza kwenye nafasi ya 17.
Meneja huyu wa zamani akipima mchango wake kwa klabu hiyo, ametoa ya moyoni kupitia tamko la Shirikisho la Mameneja wa Ligi akisisitiza kuwa “Nilishitushwa sana na kuumia na uamuzi wa kumaliza mda mda wangu dhidi ya Brighton”
Shirikisho la Mameneja wa Ligi kupitia mkurugenzi wake Richard Bevan, wsamesema kuwa meneja huyu amekuwa ni hamasa na mfano kwa mameneja wengine kwenye ligi hiyo.
Bwana huytu aliisaidia Brighton kutoka katika jinamizi la kushuka daraja League One na kufanikiwa kupambana vyema na timu bora mpaka kufikia mafanikio ya kufuzu kuingia Ligi Kuu ya Uingereza. Hata hivyo licha ya kumaliza kwenye nafasi yao ya 17, bado ameweza kujitahidi kuwasaidia kuendelea kuwepo kwenye ligi kwa msimu mwingine tena.
Chris aliteuliwa na klabu hii Disemba 2014 na sasa nafasi yake imerithiwa na Graham Potter,. Atakumbukwa kwa kuwasaidia kufanya vyema kwenye Sky Championship ambayo iliwafanya wafuzu kuingia Ligi Kuu, na msimu wao wa kwanza walimaliza katika nafasi ya 15.


Povel
Gud news