Mashindano ya Copa America yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi huku kila timu ambayo inatarajia kushiriki ikiita nyota wake ambao walikuwa na msimu mzuri kwenye vilabu vyao. Brazil ni miongoni mwa timu yenye historia ndani ya michuano hiyo na sasa wanajiandaa kwa mashindano hayo ya 49 katika historia ya bara la Amerika Kusini.
Neymar tayari ameitwa ndani ya kikosi hicho na atasaidiana na nyota wengine kurejesha ile heshima ambayo waliipoteza katika kipindi cha nyuma kwenye kombe la dunia na wanategemewa kuwa washindani wakubwa sana kwenye michuano hiyo kwa kupewa nafasi kubwa ya kunyanyua kombe hilo kwa mara ya tisa wakifanikiwa.
Adenor Leonardo Bacchi au ‘Tite’ aliyechukua mikoba ya Dunga atakiongoza kikosi chake hicho akiwa na nyota wake wanaoheshimika sana ndani ya taifa hilo kutokana na uwezo wao na viwango vyao. Mbali na hilo kuna baadhi ya nyota hawajaweza kupata nafasi pamoja na kuwa na msimu mzuri sana ndani ya klabu zao, baadhi yao ni:
Fabinho (Liverpool), suala la uzoefu linaonekana kumuweka nje nyota huyo na badala yake Fernandinho amepata nafasi ya kuungana na kikosi hicho. Ameonesha uwezo mkubwa sana msimu huu lakini hajapata nafasi ya kuingia ndani ya kikosi cha Tite.
Lucas Moura (Tottenham Hotspur), nyota wa mchezo wa klabu bingwa kati ya Spurs na Ajax ambaye alishiriki kupindua meza kibabe hajaipata nafasi ya kupenya ndani ya kikosi hicho. Alipata nafasi ya kuonesha uwezo wake kutokana na kukosekana kwa Harry Kane ndani ya kikosi lakini bado hajagusa kikosi cha taifa.
Felipe Anderson (West Ham United), alipata nafasi ya kuonesha ufundi wake akiwa na kikosi cha timu hiyo kwenye mechi za kirafiki lakini pamoja na hilo hajapata nafasi ya kukaa ndani ya kikosi cha timu ya taifa kwa sasa. Hilo linachangiwa na ushindani katika namba yake ambayo ina watu kama Philippe Coutinho na Richarlison ambao wamepata nafasi.
Vinicus Junior (Real Madrid), nyota wa Brazil anayefanya vizuri pia anategemewa kuwa mchezaji wa kipekee sana duniani. Alisajiliwa kutoka Flamengo baada ya kuonesha kiwango cha pekee na klabu yake lakini hajaonesha ushawishi bado kuwakilisha taifa lake.
Douglas Costa (Juventus), winga huyo anayekipiga ndani ya Juventus ambaye amesumbuliwa na majeraha kwa kipindi kirefu hajapata nafasi kubwa ya kucheza ndani ya kikosi cha timu ya taifa kutokana na kukosa muda mwingi wa kumuaminisha kocha. Amesugua sana benchi hadi kukosa hiyo nafasi.


Furahav
Hatari sana.
Povel
Duh hatar sana
Issa
Nzuri pia
Zeiyana
Asante kwa makala