Suala la nani atakuwa meneja anayefuata klabuni Juventus limekuwa likigonga vichwa vya habari zaidi siku za hapa karibuni. Ripoti zinamtaja nyota wa klabu hii Cristiano Ronaldo kuchagua meneja anayependa awa meneja mpya wa klabu hiyo.
Juventus wanatarajia kuachana na Massimiliano Allegri ambaye ameamua kuondoka klabuni hapo baada ya mafanikio ya miaka kadhaa. Swali kubwa ni nani ataichukua nafasi yake.
Ripoti zimekuwa zikimuhusisha aliyekuwa meneja wa Manchester United Jose Mourinho na kibarua cha umeneja klabuni hapo. Hata hivyo Carlo Ancelotti pia anatawa kuwa ni moja ya tamanio la klabu hii kuziba pengo la Allegri.
Kwa mujibu wa chapisho la Express, Ronaldo angependelea zaidi Ancelotti kuwa meneja wa klabu hiyo dhidi ya Jose Mourinho. Ronaldo anawafahamu vyema wawili hawa, ana mchukulia Mourinho kama shujaa mkubwa wa soka licha ya kutimuliwa hivi karibuni Chelsea pia Man United.
Hata hivyo, Cristiano Ronaldo hataepuka kucheza chini ya meneja mpya msimu ujao na kwa namna yeyote ile atakubaliana na meneja yeyote atakayekuja klabuni hapo.


Neema hassan
Habari njema#meridianbettz
Issa
Nzuri sana
Povel
Habar njema
aisha
Waoooooo kazi nzuri