McGregor Aonesha Ubabe Klabuni

Kati ya vitu ambavyo wanamichezo wengi wanavifanya kwa ari kubwa ni starehe baada ya kutumia kipindi kirefu kwa kutafuta mafao yao lakini inafika wakati wanazitumia visivyo kwa kuleta vurugu katika kumbi mbalimbali za starehe walimo hususan wanamichezo wa masumbwi ambao hupenda kufanya vitu kama wanavyopenda wao.

McGregor baada ya kuingia katika klabu moja ya starehe alionekana akimpiga mtu mmoja katika klabu baada ya kukosekana kwa pombe ambazo alikuwa akizihitaji. Nyota huyo ambaye kwa asilimia kubwa amekuwa akionekana kwenye klabu za starehe akizunguka na kundi la rafiki zake alifanya kitendo hicho cha wazi kabisa na kuweza kurekodiwa.

Mambo hayo yalitokea katika klabu ya Dublin ambako nyota huyo alitembelea ili kukamililisha furaha na kundi la watu wake ambao anaamini wanastahili kusherehekea mafanikio yake kwa kipindi hiki ambacho bado anasubiri mapambano ili aweze kukaa ulingoni kujenga heshima kwa mara nyingine tena.

Nyota huyo hajaingia ulingoni kwa kipindi cha hivi karibuni tangu Oktoba alipokuwa na pambano ambalo wengi walilikadiria kuwa halikuwa la kiwango chake dhidi ya Khabib Nurmagomedov. Ndani ya pambano hilo aliibuka kidedea kutokana na kumzidi mpinzani wake uwezo.

Amekuwa na matukio ambayo yanasikitisha sana ndani ya kipindi hiki na alihisiwa kwamba alichukua hata kifaa cha mawasiliano cha Ahmed Abdirzak na alilifanya tukio hilo kutokana na vilevi ambavyo alivitumia lakini kiuhalisia hakukuwa na sababu yoyote ya msingi iliyompelekea kufanya hayo yote.

Kutokana na kufanya matukio yanayoendana na hayo aliwahi kuwekwa ndani Machi 11, kutokana na tendo la kumpiga Ahmed aliyekuwa akichukua tu picha za nyota huyo akiwa na nia chanya kabisa lakini suala hilo lilichukuliwa tofauti na mkongwe huyo ndipo alipoanza kuwapiga wenzake. Kwa hali halisi mambo kama haya yanatokea kwa wengi.

Kwa sasa bado anajifua ili kuweza kurejesha heshima kwa sababu mapema Novemba atakuwa ulingoni kutengeneza heshima na kunyanyua mkanda mwingine kama akijibidiisha. Ni jambo la wakati tu kumuona kama anaweza kufikia pale panapotakiwa na kuvuka lengo.

Makala iliyopita
Makala ijayo

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.