Luis Suarez.
Staa wa soka wa timu ya taifa ya Uruguay ambaye kwa sasa anaichezea FC Barcelona ya Hispania, Ni moja ya wachezaji waliopitia msoto, akiwa na umri wa miaka 12 Suarez alikuwa akicheza mpira pekupeku kutokana na familia yake kushindwa kumudu kumnunulia viatu.
Suarez amezaliwa katika familia ya watoto saba yeye akiwa wanne na akiwa na umri wa miaka 9 baba na mama yake walitengana, Suarez wakiwa Montevideo aliendeleza kipaji chake kwa kucheza mtaani lakini pia alikuwa akifanya kazi za kufagia mtaani.


Luka Modric.
Moja kati ya viungo bora wa timu ya taifa ya Croatia na Klabu ya Real Madrid ya Hispania, lakini akiwa na miaka 6 mwaka 1991 vita vya Croatia ambavyo vilimpelekea baba yake kujiungana na jeshi, vilimfanya yeye na familia yake kwenda kuishi Kolovare katika kambi ya wakimbizi kwa miaka saba.

Carlos Tevez.
Amewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama West Ham,Man city na Man United na sasa yupo kwao Argentina anaichezea Bocca Junior.
Tevez amekulia Fuerte Apache nchini Argentina moja kati ya sehemu hatari zaidi duniani na wanaishi watu masikini na kuna matukio mengi ya kiharifu na uuzwaji wa dawa za kulevya.
Kuharibika kwa meno yake kunatokana na matukio ya ugomvi aliyokuwa anapitia katika mtaa aliokulia.

Cristian Ronaldo.
Moja kati ya wanamichezo matajiri katika hii dunia kwa sasa. Mara yake ya kwanza kupanda ndege ilikuwa ni wakati anakwenda kusaini Man United.
Kabla ya hapo Ronaldo amekulia katika familia ya kimasikini Ureno na ilifika wakati akawa analala chumba kimoja na dada zake kutokana na ugumu wa maisha licha ya kuwa umri ulikuwa unataka awe na chumba chake.

Dani Alves.
Amecheza FC Barcelona, Juventus, PSG na sasa Sao Paulo ya Brazil, Alves wakati akiwa mdogo alikuwa akilazimika kuamka saa 10 alfajiri ili kwenda na baba yake kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.
Alikuwa akilala katika kitanda kibaya, pamoja na ugumu wa maisha hayo aliyoyapitia Alves amewahi kukiri kuwa alikuwa ameridhika nayo.

Zlatan Ibrahimovic.
Ambaye ameichezea Man United,LA Galaxy ya Marekani na sasa Ac Milani ya Italy alizaliwa wilaya ya Rosengard katika mji wa Malmo nchini Sweden.
Zlatan amekuwa akiwa na sifa mbaya na ametokea katika familia ya kimasikini, baiskeli aliyokuwa anaitumia kwenda nayo mazoezini ilikuwa ya wizi.

Neymar JR.
Ambaye kwa sasa anatazamiwa kuja kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa miaka ya baadae, amelelewa katika nyumba ya babu yake ambapo alikuwa analelewa katika chumba duni sana na alikuwa akishea chumba hicho yeye, wazazi wake na dada yake.

Alex Sanchez.
Kwa kiasi kikubwa maisha yake ya utotoni amelelewa bila uwepo wa baba yake na alikuwa akifanya kazi za kuosha magari ili aweze kuisaidia familia yake nchini Chile.
Sanchez anamini kama sio mpira basi asingekuwa chochote katika hii dunia.


Frank Riberry.
Amekulia ghetto Kaskazini mwa nchi ya Ufaransa na aliepuka kuishi maisha ya bila kuwa na kazi kwa kuanza kufuata ndoto zake za kucheza mpira kitu ambacho kimemkomboa katika maisha yake na kufanya dunia nzima kumjua kwa uwezo wake.

Cheza Kasino za Mitandaoni


Samiah
Duuh
Ernest
Mafanikio bwana yanakuja kwa tabu sana, Asilimia kubwa msoto kwanzaaa baadae ndo mteremko
Njiku
Duuh mengine nilikuwa sijui aisee kama zlatan mpka baiskel ya wizi leo bonge la staa
devotha
kweli ili ufanikiwe lazima upite kwenye msoto
Povel tz
Duh kwl mafanikio ni kupamban kwl hawani kioo kwl kwetu hakun kitu cha slope kwny kutafut mafanikio thnks meridian bet kwa update za burudan na michezo
Saupha mohamed
Daah mungu ni mwema akunaanaejua kesho yeke…makala mzuri
Adelta
Ni kweli ili ufanikiwa lazima upitiy changamoto
isha
Kazi ya ustaa ni ngumu maana asilimia ya mastaa wengi wanapataga shida sana
Leonard
Msoto uliowakuza hapa walipo hawakukata tamaa
Magdalena
Mpaka kuja kumfikia mafanikio lazima upitie msoto
Lydia Emmanuel Magoti
Duu nikweli ili ufanyikiwe lazima upitie changamoto zakila dizain
Dorophina
Kweli wamepitia hali ngumu mpaka kufikia mahali pazuri
Genia Sikaluzwe
Mmh
Hamidu
Asante kwa kutuletea makala nzuri ya kusisimua#meridianbettz
Franky
Mafanikio huja na msoto so safi sana kwao
Furahav
Maisha ni safari ndefu sana.
Caroline
Hakuna kitu kinakuja Kwa urahisi
Sabrina
Maoni:Duuh wameishi maisha magumuu ila walipambana kwaajili ya kesho yao
David Pere
Wamepigia ndoto mkali lakini Sasa hivi nibmadoni kinoma na wanaheshimika kuliko hata viongozi wa nchi zao
Latifa juma mohamed
Duuh ili ufanikiwe upitie magumu
Gabriel
Nice update 👍
Sadick
Bill Gate anasema ukizaliwa masikini sio kosa lako lakini ukufa masikini ni kosa lako. wenzetu walijua karama Mungu ameweka ndani yao na wakaitumia kufanikiwa. Tatizo la wengi kushindwa ni kuridhika na hali mbaya wanayokutana nao maishani#meridianbettz
lombo
no body knows about tomorrow
farida ahmadi
Duh kupitia kipindi kigumu ndio kinaleta mafanikio katika maisha hongereni Sana wachezaji
warda
Duuuu!!!Kweli haya Maisha usikate Tamaa!#Meridianbettz
Amiri Kayera
Duh watu wanaptia changamot
Edgar
Duuh watu wanatoka mabali sana ila kwangu nimejifunza kitu kupitia mastaa hao…. Asante meridian¥
neema hassan
Maisha safari ndefu
Omary lukumbi
Duuh ina sikitisha ila pia inatutia moyo pia kwa wale ambao bado hatujafanikiwa maana uvumilivu wao ndio umefanya wapate kile ambacho walicho kiangaikia kwa muda mrefu utajir hauji kirahisi kama kutia chakula mdomoni au kusukumizia jiwe shimon
Theonestina
Hongera yao kwa uvumilivu
Salma
Chochote unachokitaka utakiwi kukata tamaa walivumilia vya kutosa na sasa wanaona matunda yake
Isaya massawe
Maisha watu wanatoka mbali kweli
Theckla
Duniani haitakiwa kukata tamaa
Revina
Mafanikio hayawezi kuja kwa miujiza lazima upambane ,ndo maana wanasema fanya kazi kama mtumwa ili uje uishi kama mfalme
David Pere
Wamepitia msoto mkari Sana lakini Sasa hivi ni madoni minimal
Amani
Asilimia kubwa msoto kwanzaaa baadae ndo mteremkoTatizo la wengi kushindwa ni kuridhika na hali mbaya wanayokutana nao maishani#meridianbettz
Fatuma kasomo
Hongera kwa uvumilivu
Tatu
Mafanikio ayaji kwa njia rahisi
Ester jackson
Ni historian ya kusisimua ambayo ina mafunzo ndani yake kuwa masikini katika familia sio mwisho wa maisha ni hakili na juhudi katika nia uliyo iweka asante meridian kwa nakala
Khadija
Nimekubali kweli haya maisha usikate tamaa#meridianbettz
Zeiyana
Ronaldo amepitia maisha magumu sana kuna badhi ya maisha uwezi kuyasahau katika histor yako kwa kweli
felister
mafanikio bwana yanakuja kwa tabu sana
Rehema
Duuu!
Shafii
Siku zote wanao pambana ndio wanaofanikiwa.
JULIANA
Asante kwataharifa,maana nimejua nisiyoyajua
Hope mwaikuka
Nlkua sijui hii axante kwa kunijuza
tumaini
Maoni:mtafutaji achoki
Flomena
Mafanikio bhana ni Kama dhahabu ichomwe kwenye Moto ndio ing’ae