Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa wachezaji wote wanapaswa kutumia maneno ya Paul Pogba kama hamasa katika mapambano ya kutwaa taji la Premier League.
Man United wamefanikiwa kufikisha mfululizo wa mechi 17 sasa bila kupoteza baada ya kupata ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Aston Villa Alhamisi.
Pogba alizungumzia mpango wa Man United ulikuwa ni kutwaa taji, kitu ambacho kwa mara ya mwisho wamefanikiwa msimu wa mwaka 2012/13.
Meneja Ole Gunnar kwa upande wake anaamini kuwa klabu inaweza kurejea kuwa vinara wa EPL, lakini anasema itakuwa mda gani hilo ni suala la wachezaji kuamua. Jitihada za kila mwanatimu zitaleta mabadiliko kikosini na kwenye ligi.
“Nina uhakika tutapita changamoto hii na kurejea kuongoza kwenye ligi… Tumeendelea kuwa bora kama timu, tunatakiwa tukumbuke tumetoka mbali sana msimu huu.”
Akisisitiza nafasi ya kila mchezaji, alimtumia Pogba kusema kuwa maneno yake yanatakiwa kuchukuliwa kwa uzito kama hamasa katika mapambano ndani ya EPL na bila shaka watatoboa.
Unafurahia kubashiri michezo gani?
Yote unaipata hapa Meridianbet


warda
Kweli Kabisa Pogba Anatia Hamasa Sana Nawapenda Man U#Meridianbettz
Lydia Emmanuel Magoti
Yah yupo vizuri Pogba anajua anacho kifanya
Ester jackson
Yupo sasa kocha anajua anacho kiwaza pogba
Mwanahamisi
Pogba namkubali sana
Sylvester
Ni Changamoto kubwa waliyoipia toka msimu wa 2012/2013 kwa kutwaa mataji,imekua misimu wa timu kuwa bora kwa kupanda na kushuka kusipokua na mpango maalumu ila kwa kikosi cha sasa na uwepo wa Ole nina imani msimu ujao Manchester itakua moto wa kuotea mbali na kuweza kushika nafasi ya kwanza na kutwaa ubingwa tena.
Zeiyana
Mashetani wekundu wana mlali sana msimu huu ukiangalia ni kweli changa moto kubwa waliyo pitia man united ulikua kutwaa taji ni kitu amabacho kwa mara ya mwisho wamefanikiwa msimu wa mwaka 2012/2013
Adelta
Pogba namkubal Sana
Ni mtu anayejitambua sana
Sadick
Tangu wakati ule hapa katikati mambo yamebadilika sana.Man City na Liverpool zimepata Waalimu na Wachezaji wazuri wakati huo Man U ilikosa muunganiko huo. Kwa sasa kuna wachezaji wazuri kunahitajika Kocha kuwa na hamasa na nguvu ya kufanya kazi yake yote yatawezekana kurudia enzi za ushindi na kubeba makombe#meridianbettz
Dorophina
Ndiomaana mashabiki wa man u hatutaki pogba haondoke anajua nn anakifanya kwenye timu na anamchango mkubwa tu
felister
big up pogba
Theckla
Yuko sahihi
Neema juma
Pogbaa ni mfano wa kuigwa namkubalii mno
Revina
Ni kweli kabisa Pogba ndiye Hamasa man u ,na sasa Man u ya sasa inakaribia kuwa kama ile ya mzee Alex
Mariam mtandama
Pogba anajitambua na yupo vizur
Latifa juma mohamed
Anajitambua na mfano wa kuigwa pogba
Magdalena
Pogba amekuwa ni mtu mwenye uwezo wa tofauti Sana katika mpira na ndie mchezaji mwenye kujituma Sana apo United
Rehema
Ni kweli Yuko vizuri na ndio maana mashabiki wa man u wanapenda pogba aendelee kubaki man hii wabebwa vizuri
Caroline
Pogba amekua mfano wa kuigwa
lombo
saf
Hamidu
Kiungo fundi hatabaki kuwa juu muda woteeeeeeee yajao yatafurahisha
Genia Sikaluzwe
Fundi anajuwa Sana kujituma anapo kuwa uwanjani
Tatu
Pogba anajituma sana
Shafii
Habari njema kwa wana man u.
mwajuma
Namkubali sana pogba na anatia amasa kweli #Meridianbettz
JULIANA
Anaepinga anifuate, Pogba mashine
Njiku
Paul lamile pobga ni mchezaji mzuri sana na anahamasa akiwa uwanjani pia anajituma sana na analeta matokeo akiwa uwanjani tangia kurudi kwake man u kutoka kwenye majeruhi man u inafanya vizuri zaid na combination yake yeye na bruno ipo poa sana kupambana ili kuikamata top4,
Franky
Ana jambo uyoo
Sabrina
Maoni:Paul Pogba mkali wao
Ernest
Pogba leo anaonekana shujaa wakati miezi mitatu nyuma alikuwa akitupiwa maneno machafu, Me binafsi natamani kuona Pogba akitimka ndani ya Man U.
neema hassan
Asante kwa makala
Samiah
Good
Gabriel
Kwel kabisa
Issa
Pogba anajua ni swala la timu kukaa pamoja kuelewana
Saupha mohamed
Safi pogba
farida ahmadi
Kweli kabisah Pogba ni mchezaji mzuri Sana na ameisaidia man United kwa kiwango lazima kocha wake aseme ukweli
Edgar
Kweli kabisa maana nw mambo yamekuwa mazuri kabisa kwa man u.. na hii yote inatokana na combination nzuri ya pogba na Bruno.. so pongezi kwake pogba
Tahiya
Ni vizur kuwa na imani na timu yake watafika wanakotaka
devotha
Pogba mfalme ajaye old traford
Hope mwaikuka
Sawaa
Omary lukumbi
Ole gunnar amekua na furaha sana kwa kiwango cha timu mzima na jitihada za mchezaj mmoja mmoja pogba na bruno na wachezaj wengine wameirudisha United kwenye uhai tena
David Pere
Hamasa ipo kwelikweli Ndio maana anazidi kufanya vizuri
Zuhura omary kindamba
Pogba ni mchezaji mzuri
mwakalosi
huyu alikuwa anatusumbua kila siku anataka kuongezewa mshahara huyu ole asilete ujinga sasa ataondoka na pogba wake
Flomena
Nina uhakika tutapita changamoto hii na kurejea kuongoza kwenye ligi… Tumeendelea kuwa bora kama timu, tunatakiwa tukumbuke tumetoka mbali sana msimu huu.
Povel tz
Kocha anaonekana ana mahaba na labile Pogba
Amiri Kayera
Pogba anaujua san
Salma
Kwel kabsaa