Conte: Naweza Kuendelea na Inter au Nikasepa.

Antonio Conte amekuwa na shaka kama ataendelea kuwa kocha wa Inter Milan baada ya kushindwa kupata taji la Europa League kwa kucharazwa 3-2 na mabingwa wa mashindano hayo klabu ya Sevilla siku ya Ijumaa.

Romelu Lukaku alianza kuipatia goli la kuongoza Inter goli alililofunga kwa mkwaju wa penati kipindi cha kwanza kabla ya Luuk de Jong hajaiswazishia timu Sevilla kipindi hicho hicho cha kwanza.

Hii inamaanisha The Nerazzurri walikuwa wakijaribu kukamilisha msimu kwa kuwinda kombe hilo kama walivyofanya kwenye Serie A kwa kumaliza msimu wakiwa na matokeo mazuri na kuwa katika nafasi ya pili kwa tofauti ya alama 1 nyuma ya Juventus lakini bahati haikuwa kwao wamekosa ubingwa wa Ulaya wakiwa chini ya Conte.

Na kocha huyo wa zamani wa vilabu kama Chelsea, Juventus na timu ya taifa ya Italia amesema huenda asiendelee kuinoa timu hiyo.

“Tutakutana wiki ijayo na bodi ya klabu na kuamua juu ya mustakabali wangu. Sina uhakika kama nitakuwa kocha wa Inter msimu ujao, tutaamua kwa pamoja. Inter itapanga mipango yake ya siku zijazo… “

Antonio Conte na bodi ya Inter watakutana wiki ijayo kufanya uamuzi juu ya hatma yake na endapo atafungshiwa vilago klabuni hapo, kocha wa zamani wa Juve Massimiliano Allegri ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuwa meneja mpya wa Inter.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi ucheze

39 Komentara

    Conte mbona ni kocha mzuri tu.kukosa taji la Europa isiwe sababu ya kumfukuza

    Jibu

    Kulikuwa na uvumi kabla ya fainali kwamba kama Inter haitashinda kombe lolote basi Conte angetimuliwa. Bodi inapaswa kumupa muda aweze kuonyesha makali yake#meridianbettz

    Jibu

    Maamuzi unayo wewe tuu kuendelea kubaki inter hau kusepa#meridianbettz

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Inter wamepambana sana msimu huu lakini bahati haikuwa yao, ni wakati kwa uongozi wa Inter kuangalia tena swala la Conte

    Jibu

    Maamuzi anayo mwenyewe

    Jibu

    Inter naona wanataka kutimiza ahadi yao ya kutaka kumfukuza Conte wamuangalie msimu ujao atafanya nn

    Jibu

    ngoja tuone uamuzi wao watakapokutana iyo wiki ijayo tujue atma ya conte

    Jibu

    Me sioni uwezekano wa kuondoka kocha conte ni bola wangempa mda mwengine tu ukiangalia kuna mengi kayafanya kwenye clabu hiyo jitihada zake alizo fanya hadi kuipelekea kushiriki taji la Europa league ametuonesha kabic hana weza wangempa mda tu

    Jibu

    inter wasifanye maamuzi ya kukurupuka maana konte ana mchango mkubwa sana pale kapambana mpaka timu kufika fainal ingawa awajachukua ubingwa

    Jibu

    Muhim kujipanga msim ujao

    Jibu

    Inter mpeni muda conte ili.afanye maujuzi yake mbona yuko vizuri

    Jibu

    Maamuzi anayo mwenyew#Meridianbettz

    Jibu

    Mahamuzi ni yake kubaki kuondoka!

    Jibu

    Conte asifanye jambo kwa hasira wakae chini waangalie wapi walipokosea wajipange upya msimu ujao

    Jibu

    Akipewa muda atatoa maamuz mazuri

    Jibu

    Bora uendelee kubaki Inter kwani umejitahidi kutengeneza kikosi kizuri chenye ushindani kwa sasa ingawa haikua nahati yako kutwaa Europa jana

    Jibu

    Kuondokaa sio kuondoa tatizo abaki2

    Jibu

    Uwamuzi niwake kubaki hau kuondoka Conte kwa mm naona haendere tuu hapo hapo lnter

    Jibu

    Maamuzi anayo mwenyewe abaki au aondoke

    Jibu

    Konte kuondoka inter ni mapema jenga timu ili msimu ujao utawale seria a

    Jibu

    Maamuzi ni yake

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Antonio Conte n kocha mzur sana nakubaliana mfumo wake Jambo la kushinda au kushindwa n matokeo ya kawaida sana na n matokeo ya bahati tu

    Jibu

    Ww tu na maamuz yako

    Jibu

    Maamuz ni yake kusalia au kubaki Milan

    Jibu

    Amua lililosahihi kwako

    Jibu

    Uwamuzi uko kwake conte kusepa au kusalia.

    Jibu

    Wewe tuuu na roho yako!!!!

    Jibu

    Kulikuwa na uvumi kabla ya fainali kwamba kama Inter haitashinda kombe lolote basi Conte angetimuliwa. Bodi inapaswa kumupa muda aweze kuonyesha makali yake

    Jibu

    Kocha mzur tu

    Jibu

    Kwa uwezo alio kuwa nao kucha na kuifikisha mbali timu hiyo in bora angebaki bado anastahili kuitumikia kalbu hiyo conte hata kama walikosa ubigwa bana kunanafasi mbeleni kuwa bora zaidi

    Jibu

    Maamuzi yake binafsi mwenyewe Conte to

    Jibu

    Kocha makini sanaaa

    Jibu

    Conte bado yuko vizuri.

    Jibu

    Conte nie kocha mzuri tu asihofu kuondoka inter Bado anahitajika hapo inter milan

    Jibu

    Conte ni kocha mzuri hakupaswa kuchukua hasira mkononi baada ya kupata kipigo ni vema angeangalia wapi wamekosea.

    Jibu

    Conte nae anatamba sana ndo mana kafugwa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.