Mchezaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal Danny Welbeck amejiunga na klabu ya Brighton and Hove Albion.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aliachana na Watford mwishoni mwa msimu uliyopita, sasa amesaini dili ya mkataba wa mwaka 1 na timu aya Graham Potter.
Anaweza akaanza kucheza mechi yake ya kwanza katika Premier League dhidi ya West Brow siku ya Oktoba 26.
“Tunafuraha kuwataarifu kwamba Danny Welbeck amejiunga nasi, atatusaidia katika safu ya ushambuliaji,” Potter alisema kupitia tovuti ya Brighton.
Welbeck alianza katika michezo tisa pekee kwenye Premier League katika misimu miwili iliyopita na amekuwa akikabiliana na majeraha miaka ya hivi karibuni.
United ambao ni mabingwa wa Premier League 2012-13 ndiyo klabu ambayo Welbeck alijiunga nayo lakini mwaka 2014 alitimkia Arsenal baada ya kuonekana kutokuwa chaguo namba moja katika mipango ya kocha Louis va Gaal.
Alifunga magoli manee na kutoa asisti tatu katika michezo 27 katika msimu wake wa kwanza na Arsenal pia alifunga dhidi ya klabu yake ya zamani United na kuwatoa kwenye FA Cup mchezo uliyopigwa Old Trafford lakini baada ya wiki kadhaa katika msimu alipata jeraha la goti na kufanyiwa upasuaji.
Baada ya Mkataba wake kufika mwisho mwaka uliyopita, alijiunga na Watford na kufunga magoli matatu katika michezo 20 kwenye mashindano yote.
Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua.



Povel
Kila la kheri DANI welbeck
Issa
Welbeck hana bahat
Janeflora malisa
Vzr
Amiri Kayera
Tunamwombea kher atakua kiwango
Sauda
Kazi kazi kijana.
Fatuma kasomo
Gud
aisha
Kila la kher welbeck
Rehema
Safi
Sabrina
Piga Kazi Welbeck
zeiyana
mda wake sasa welbeck wa kuonesha mahajabu yake
Adelta
Welbeck Yuko vizuri tunasubiri tuone maajabu yake
Angelina
Kila kheri kafanye maajabu
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri kijana kila la Kheri kwenye utendaji wako wakaz
Fatina mfingi
Safii kijan kwa kazi nzuri
magdalena
kila la kheri kijana ingawa bado safari ya mafanikio yako imekuwa ndefu sana
latifa juma mohamed
Vema zaidi, deal done.
Tatu
Kijana yupo vizuri kila LA khery
Khadija
Kazi kazi kijana
Mwajumah
Kila la kheri kijana
Elika
Safi sana
Shani
Welbeck mchezaj mzur sem han bahati
Fatuma kasomo
Safi sana
Hopemwaikuka
Sio mbaya
Gabriel
Welbeck mchezaj mzur
warda
Hongera yake