Bruno Fernandes amesema kwamba mchezaji wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka aliwashtua baada ya kufunga kwa shuti kali alililopiga kwenye mchezo dhidi ya Newcastle United, amesema: “Hatukujua kama ange piga shuti pale!”
Beki huyo alicheza mechi yake ya 50 kwa Manchester United na kufanikiwa kufunga goli lake la kwanza katika klabu na kuibuka na ushindi wa 4-1 siku ya Jumamosi katika dimba la St James’ Park.

Fernandez ilikuwa afunge goli la mapema baada ya kupiga penati ambayo mlinda lango wa Newcastle aliizuia na hii ilikuwa penati namba 11 kwa mchezaji huyo tangu ajiunge na United katika mechi hiyo Harry Maguire aliokoa mpira ambao ulikuwa wa kujifunga kutoka kwa Luke Shaw.
Wan-Bissaka aliweka kamba ya 3 baada ya kufanya shambulizi kwa kupasiana na Marcus Rashford, ambaye aliongeza chuma cha nne baadaye.
Lilikuwa goli la kwanza kwa beki huyo katika Premier League baada ya michezo 80 katika mashindano, amejaribu kupiga mashuti 18 ambayo hayakuelekea langoni na kufanikisha mashuti matatu ambayo yalielekea golini.
Fernandes amesema alikuwa akimtania Wan-Bissaka katika vyumba vya kubadilisha nguo, kwa kumuambia goli lako lilikuwa ni krosi mbaya uliyokosea.
“Hatukujua kama ange shuti!” alisema kupitia MUTV. ” Ni ngumu kuamini kama angefunga kwa sababu hatujawahi kumuona akipiga mashuti.
“Tulikuwa tukimtania katika vyuma vya kubadili nguo, tulisema wote tulikua tunajua anataka kupiga krosi na ile alikuwa amekosea na bahati nzuri akafunga.
“Kila mtu anajua kwamba Wan- Bissaka ni mlinzi lakini anaweza akaonesha zaidi kwamba pia ni mshambuliaji, nadhani ana ubora wa kufanya hivyo.
Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua.



Issa
Wana bisaka hafai
Amiri Kayera
Ni beki mzur Ila kunamamb kidg aongeze awe bola
zeiyana
kwa uwezo aliokua nao kama watampata nafasi ya kutosha pale clabuni naimani mengi tutayaona wan bissaka alionesha uwezo aliokua nao
Adelta
Ni beki mzuri Ila aongeze juhudi ktk majukumu yake
Angelina
Yuko vizuri
Lydia Emmanuel Magoti
Mtuwakaz wa Man U anajua
Fatina mfingi
Atafany mengi makubwa kikubw wampe ushirikiano wa kutosha
latifa juma mohamed
Kila mtu anajua kwamba Wan- Bissaka ni mlinzi lakini anaweza akaonesha zaidi kwamba pia ni mshambuliaji, nadhani ana ubora wa kufanya hivyo.
magdalena
kijana alionesha ufundi wa hali ya juu sana mpaka kuipatia united ushindi
Tatu
Ni beki mzuri
Khadija
Nakala pendwa
Mwajumah
Ni beki mzuri sana
Elika
Yupo vizuri
Janeflora malisa
Safi
Shani
Wan bissaka bek makin
Fatuma kasomo
Yupo vizuri
lombo
duuh
Povel
Bonge la makala
aisha
Yuko viziri sana
Hopemwaikuka
Namuelewa sana
Gabriel
Ni beki mzuri
Saupha mohamed
Jamaa yupo vizur
Sabrina
Wan-Bissaka fundii
farida ahmadi
Yuko vizuri Sana
Sauda
Anajitahidi