Neymar Kushtakiwa na Barcelona?

Klabu ya Barcelona imeripotiwa iko mbioni kumshtaki nyota wake wa Zamani Neymar kwa kile wanachokiita ni kumzidishia malipo kwa zaidi ya Euro milioni 9 alipokuwa Barcelona.

Inakumbukwa nyota huyu wa PSG tayari alishalazimishwa kurejesha takribani Euro milioni 5.9 ambazo pia zilionekana kuwa ishu kwenye masuala ya bonasi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa The Sun, Barcelona walifanya hesabu vibaya za makadirio ya malipo ya Neymar na Kodi kwa miaka miwili ya awali na kujikuta wakilipa zaidi ya ilivyotakiwa.

Taarifa zaidi zinaripoti Wakala wa Kodi wa Barcelona tayari wametoa neno kwa Barcelona kuwa ikiwa watashindwa kufikia muafaka suala hilo, basi €9m itachukuliwa kama ni pesa ‘waliyojitolea kwa Neymar’ kama zawadi tu.

Huu ni muendelezo wa migogoro iliyoripotiwa kati ya pande hizi mbili. Mwezi Januari, Neymar aliripotiwa kuwa yeye ndiye anawashtaki Barcelona kwa takribani €3m – ambazo ni sehemu ya mshahara wake ambayo haijalipwa.

Baadala yake, taarifa mpya zinawataja Barcelona wakitaka kurejesha mara tatu ya pesa ambayo Staa huyu alitajwa kudai.

Sakata hili kwa upana wake linaihusisha na klabu ya Santos, ambayo Neymar aliondoka kuelekea Barcelona. Sekeseke hili pia halimuachi salama aliyekuwa raisi wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anayeshutumiwa kwa udanganyifu wa kodi na rushwa.

Suala hili linaibuka wakati Barcelona wakiwa wanajaribu kuweka sawa vitabu vyao vya fedha baada ya kupata changamoto kubwa ya kiuchumi kutokana na janga la Corona.


 

UMEJARIBU HII POKER YA VIDEO?

Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!

Meridianbet Casino

INGIA MCHEZONI!

21 Komentara

    Barcelona waache ubabaifu walipe tu kumaliza kesi

    Jibu

    Barca wanayumba kama makosa waliyafanya ni wao wenyewe kwaiyo ni kazi bure kumshtaki neymar

    Jibu

    Barcelona sasa wanafika mbali sana..wakae wayajenge

    Jibu

    Barcelona Hawana haja ya kumshitaki sababu kama makosa waliyafanya wenyewe yeye hakuiba

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Inakuwaje sasa kwa upande wa neymar

    Jibu

    Hawamfanyii khaki kabsaa wamalizane tu

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Barcelona walipo fika sio pow bora wakae tu wayajenge

    Jibu

    Swala la pesa kwa Neymar sio tatizo.ni kitendo cha kukaa mezani na kuyamaliza

    Jibu

    Duuh ndio yamekua hayooo

    Jibu

    wamalizane tu jamaniii

    Jibu

    Asnt kwa taarif

    Jibu

    Barcelona mmepotea sasa mnaaza sababu nyingine tu hizo zisizo na mashiko siku zote hizo mlikuwa wapi hasaivi ndio mnamuona yuko vizuri ndio mana mnaingiza maneno yenu muacheni nerymaa ale good time yake vema

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Neymar ni malipo yasiyo hak kwa timu yk

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Hiyo wafanye tu kama bonus zake kipindi alichokupo clabuni hapo wasitengeneze chuki na wachezaji hitajenga twasira mbaya kwenye clabu yao

    Jibu

    Nice information

    Jibu

    Neymar ni mwanzo tu ila barca itamuandam sna kwa sababu ilitumia gharama nying pasipo kufaidika nae

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.