Anthony Joshua Awasaidia Mabondia Wachanga.

Baada ya kufanya vizuri na kujitengenezea jina kubwa kwenye ulimwengu wa ndondi, bondia Anthony Joshua amejitolea kuwasaidia mabondia wachanga nchini Uingereza.

Anthony Joshua ameamua kuwashika mikono mabondia wanaochipukia akiamini kuwa anajukumu la kuwaendeleza watoto na vijana wa kizazi kijacho.

Kwa kuamini hilo, AJ ametoa mtonyo mrefu na kuahidi kujitolea kufanya mazoezi na mabondia wachanga kama sehemu ya kuwapatia motisha na kuamini chochote kinawezekana.

Akizungumza na Dan Roan wa BBC Sport, AJ amesema “bila ya kuwa na mashindano ya chini, hakuna Anthony Joshua. Milango ya sehemu hizi za mazoezi ipo wazi kwa mabondia wote wachanga kutoka kwenye mazingira yeyote.

AJ akiwa na mikanda aliyoipata kwenye mchezo wa ndondi mpaka sasa.

“Kama ningeweza kurudi kwenye miaka 18 na sehemu zote za mazoezi ziwe zimefungwa kama hivi, ningevunjika moyo sana.

“Sio msaada wa fedha tu. Nitajitahidi kuwapa motisha hawa watoto kwa kuwa sehemu yao, nitashusha mikanda yangu na kufanya nao mazoezi. 

“Ninaamini katika miaka 10-15 ijayo, tutawaona viongozi wa kesho, lakini siamini kama ni miaka 25-30 kwasababu tumeshakipoteza hiki kizazi.”

AJ baada ya kung’ara kwenye mashindano ya Olympic 2012.

AJ aliianza safari yake ya kuwa bondia mkubwa duniani baada ya kushinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olympic 2012 wakati ule akiwa kama bondia mchanga.

2016 AJ alikuwa bingwa wa dunia baada ya kumburuza Mmarekani – Charles Martin ambapo aliibuka na mkanda wa IBF.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

14 Komentara

    Ni miongoni mwa mabondiya wanaopenda kuona mafanikio ya wenzao

    Jibu

    Ni jambo zuri

    Jibu

    Safi ni uamuzi mzuri

    Jibu

    Safi sana niuwamuzi mzuri

    Jibu

    Jambo jema

    Jibu

    Jambo zuli

    Jibu

    Joshua anajitoa sana

    Jibu

    God bless you

    Jibu

    Jambo zuri

    Jibu

    Jambo zuri

    Jibu

    Jambo jema

    Jibu

    Safiii Sana kafanya Wema zaidi kwa ware wanao taka kuinuka zaidi

    Jibu

    Ndo vizuri

    Jibu

    Jambo zuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.