Burudani ya ligi ya NBA mara zote inaendana na kufikiwa/kuwekwa au kuvunjwa kwa rekodi kadha wa kadha. Jumatatu hii, Stephen Curry ameweka rekodi ndani ya timu yao ya Golden State Warriors.
Licha ya Warriors kutokuwa na matokeo mazuri msimu huu, Stephen Curry ameendelea kuwa mchezaji anayeonesha juhudi na uwezo binafsi ndani ya kikosi hicho. Jumatatu hii, Warriors walikuwa uwanjani kupepetana na Denver Nuggets.
Kabla ya mchezo dhidi ya Warriors, Nuggets walitoka kufungwa na Boston Celtics na jumatatu hii wameambulia kipigo cha pili mfululizo mbele ya Warriors.
Curry ambaye alipachika pointi 53, hii ni mara yake ya 9 kufunga zaidi ya pointi 50 na ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote ndani ya kikosi cha Warriors akiwa na jumla ya pointi 17,818.

Curry alijiunga na miamba hii ya NBA (Golden State Warriors) mwaka 2009. Katika mchezo wa Jumatatu, aliisaidia timu hiyo kupata ushindi kwa pointi 116-107. Kufuatia rekodi hii, baadhi ya wachezaji waliowahi kucheza ligi ya NBA wamempatia majina Curry.
Reggie Miller amempatia Curry jina la “Mr Warriors” wakati Andre Iguodala wa Miami Heat anasema Curry ni “Mungu”
Kwingineko kwenye NBA Jumatatu hii, Washington Wizards wamewatoa umaarufu Utah Jazz ambao walikuwa wameshinda michezo 24 (125-121). Philadelphia 76ers wamewafunga Dallas Mavericks (113-95). New York Knicks wamewafunga LA Lakers (111-96).
Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



warda
Curry anajua sana