Katika ubora wake hakuna ambacho kingemzuia Kaka akiwa na mpira mguuni, ushuhuda wanao mabeki na viungo waliokabiliana nae akiwa na uzi wa AC Milan msimu wa 2006-07.
Wapinzani Italy na Ulaya nzima walikiri hakukuwa na binadamu anaeweza kuuamuru mpira kama yeye. Ni kama aliona njia za mpira mara mbili zaidi ya binadamu wa kawaida.
Alikuwa ubongo, moyo na pumzi ya AC Milan. Naizungumzia AC Milan yenye Gennaro Gattuso na Andrea Pirlo katikati. Subiri kwanza nikueleze mechi fulani iliyocheza miaka 14 iliyopita.

Siku hiyo AC Milan wamesafiri kwenda Old Trafford kuivaa Manchester United ngumu ya Sir Alex Ferguson, kila mtu alikuwa na imani na Man United.
Kwanza Man United walitinga nusu fainali kibabe wakiiondosha AS Roma. Upande wa pili, AC Milan walikuja nusu fainali kwa tabu, baada kuvuja jasho na damu mbele Bayern Munich.
Man United walipata bao mapema sana kupitia Cristiano Ronaldo. Wakiwa na faida, waliendelea kuwasaka Milan. Wakiwa bize kushambulia, walisahau kuna hatari iliyobebwa upande wa pili na miguu ya mtoto fulani kutoka Sao Paolo Brazil.

Bao la kwanza lilikuja dakika ya 22, Clarence Sedorf alimpa Mpira Kaka, kwa haraka Kaka alimuacha Gabriel Heinze, kisha akasafiri hadi pembeni ya box na kumtungua Van der Sar kwa shuti la mguu wa kushoto, kistaarabu sana.

Bao la pili ndilo lililowanyanyua hadi mashabiki wa United kwenye viti. Fergie na ujanja wake akaishia kupiga makofi kwasababu hakuamini alichokiona.
Kaka akiwa mbele ya wachezaji wa watatu ya United, alichezewa mpira mrefu mashariki mwa uwanja, akampunguza Darren Fletcher kwa mwili, kisha akamuita Heinze na Evra, akawadanganya na kuwagonganisha.
Hakuishia hapo, na jezi yake namba 22 mgongoni akamtungua tena Van der Sar lakini safari hii ilikuwa kwa mguu wa kulia. Hadi mtangazaji Clyve Tyldesley alikaukiwa maneno. Akaishia kusema tu, “Completely magical.” Hata hivo angesema nini kingine??

AC Milan walitinga fainali baada ya mechi ya pili na walienda kutoa ndoo yao ya saba ya Ulaya.
Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.



Magdalena
Kijana mahili Sana kwa united
Khadija
Yuki vizuri
aisha
Safi sana
Adelta
Good
Lydia Emmanuel Magoti
Safiii sana
neema hassan
Asante kwa taarifa
Khadija
Safi sana
warda
kITAMBO SANA