Copa America 2021 Yaanza, Brazil Yang'aa

Michuano ya Copa America imeanza kutimua vumbi usiku wa kuamkia leo huku Brazil, na wenyeji hao hao wameanza vyema sana kwa ushindi wa 3-0.

Michuano hii ilipitia misukosuko sana kufuatia suala la Covid 19 huku nchi mwenyeji zikibadilishwa mara kadhaa kutokana na janga hilo.

Wachezaji wa watatu wa Brazil, Neymar, Marquinhos na Gabriel Barbosa wote walifunga magoli katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Venezuela ambao wachezaji wao 12 kati ya 26 walioitwa walikutwa na Corona.

Brazil ilikuwa nchi mwenyeji wa mashindano hayo wiki moja iliyopita baada ya Argentina na Colombia kuondoshewa uenyeji huo kutoka na suala hilo hilo la Corona.

Ushindi huo wa 3-0 kwa timu ya Brazil yenye mastaa kibao wa soka ulikuwa mwanzo mzuri huku nahodha wa timu hiyo, mchezaji wa Real Madrid, Casemiro akidai kuwa wana kila sababu ya kushinda taji hilo.

Timu ya Venezuela ililazimika kuleta wachezaji wapya 15 baada ya waliokuwa kwenye kambi 12 kupatwa na matatizo hayo ya Covid.

Katika ushindi huo, Nyota wa PSG, Neymar alifunga moja na kutoa assisti moja na Marquinos alifunga moja kwa mpira uliokufa!


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

3 Komentara

    Always Brazil wako vzur

    Jibu

    Wako vizuri

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.