Tiketi za pambano la Anthony Joshua bingwa mtetezi wa ubingwa wa (IBF, WBA, WBO na IBO) dhidi ya Oleksandr Usyk kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur huko London Jumamosi Septemba 25 zimeisha ndani ya masaa 24 ya kwanza ya kuuza.

AJ amewahi kuuza tiketi zote katika kumbi na viwanja vya michezo huko Uingereza, USA na Saudi Arabia hapo awali na sasa yuko tayari kurudi mji mkuu wake kwa pambano lake la tano la uwanja nyumbani Spurs.
Zaidi ya mashabiki 100,000 walisubiri kwenye foleni ya kununua tiketi StubHub kwa nafasi yao ya kupata viti kwa mpambano mkubwa zaidi wa mwaka wa uzani mkubwa na nyota wawili wa medali za dhahabu za Olimpiki za London 2012.
Joshua (24-1, 22 KOs) alitawala kwa kumpiga Kubrat Pulev na kupata ushindi wa kikatili wa raundi ya tisa katika Uwanja wa SSE, Wembley mara ya mwisho mwezi Desemba katika pambano lake la kwanza kwenye ardhi ya Uingereza tangu alipomchapa Alexander Povetkin katika raundi saba kwenye Uwanja wa Wembley mwezi Septemba 2018.
Nyota wa Ukraine Usyk (18-0, 13 KOs) alihamia kwenye uzani mzito baada ya kutawala katika cruiserweight, akimaliza kiengo chake kwa 200lbs bila kupoteza, kwa ushindi dhidi ya Marco Huck, Mairis Briedis , Murat Gassiev na Tony Bellew.
Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!



Sania+mapua
Pambano Kali sana hili