Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Barcelona ina matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba katika uhamisho wa bila malipo msimu ujao iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ataamua kutotia saini kandarasi mpya pia PSG , Juventus na Real Madrid zinavutiwa na mchezaji huyo.

Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner ,25, ni miongoni mwa wachezaji wanne wanaonyatiwa na Borussia Dortmund iwapo mshambuliaji wao klabu hiyo Erling Braut Halaand ataondoka katika klabu hiyo msimu ujao.

Tetesi zinasema, Kandarasi ya beki wa Ujerumani Antonio Rudiger katika klabu ya Chelsea inakamilika msimu ujao na mazungumzo ya kuiongeza yamegonga mwamba.

 

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anatarajiwa kumpandisha kiungo wa kati wa timu ya wachezaji chipukizi katika klabu hiyo Charlie Patino katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku kukiwa na ripoti kwamba klabu ya Barcelona inamnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 wa England.

Mmiliki wa klabu ya Fiorentina Rocco Commisso hajui iwapo mshambuliaji wa Serbia mwenye umri wa miaka 21 Dusan Vlahovic , ambaye amehusishwa na klabu ya Manchester City , Atletico Madrid na Juventus , ataongeza mkataba wake zaidi ya mwezi juni 2023 na klabu hiyo ya Italia.

Naibu mkufunzi wa Newcastle Graeme Jones na mshambuliaji wa England Dwight Gayle, 30, walirushiana maneno makali katika uwanja wa mazoezi huku nahodha Jamaal Lascelles akilazimika kuingilia kati na kuwatawanya wawili hao.

 

Koemann: Luuk de Jong ni Hatari Kuliko Neymar

Tetesi zinasema, Mkufunzi wa Everton Rafael Benitez amepatia kipaumbele kumsajili beki wa kati katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.

Baadhi ya wanachama wa bodi ya klabu ya Barcelona wamemtaka rais wa klabu hiyo Joan Laporta kumfuta kazi mkufunzi Ronald Koeman baada ya kulazwa 3-0 na Bayern nyumbani.

Tetesi zinasema, Tottenham ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Borussia Monchengladbach Matthias Ginter lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich na Real Madrid ili kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Ujerumani.


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.