Tetesi zinasema, Barcelona wanajiandaa kuwasilisha ofa za kuwanunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, nyota wa Ufaransa na man united Paul Pogba, 28, na mchezaji wa Uhispania Dani Olmo, 23.
Tetesi zinasema, Kiungo Jesse Lingard, 28, na beki Eric Bailly, 27, ni miongoni mwa wachezaji saba ambao wanaweza kuuzwa na Manchester United mwezi Januari.
Tetesi zinasema, Chelsea itakabiliana ana kwa ana na Juventus kupata saini ya kiungo wa chini ya umri wa miaka 21 wa Ufaransa na Monaco Aurelien Tchouameni, 21, mnamo Januari.

Tetesi zinasema, Liverpool, Tottenham, Chelsea na Juventus wamepania kupigania winga wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman, 25.
Bosi wa Barcelona Ronald Koeman hajui hatma yake iko vipi wakati kukiwa na ripoti kwamba rais Joan Laporta anaunda orodha ya watu wanaochukua usukani wa klabu.
Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 28, anaweza kuwa bado anahisi athari za uhamisho wake ulioshindwa kufanyika wa Manchester City msimu huu wa joto.
Juventus walikuwa wamepanga kumsaini Gianluigi Donnarumma, 22, bila malipo kutoka AC Milan msimu huu wa joto, lakini walilazimika kujiondoa kwa sababu za kifedha, na kuiruhusu Paris St-Germain kumchukua.

Mkurugenzi wa michezo wa PSG Leonardo amepuuza maoni kwamba nyota wa Argentina Lionel Messi, 34, atapata zaidi ya pauni milioni 30 kwa msimu wakati wa mkataba wake wa miaka mitatu.
Tetesi zinasema, Arsenal inaandaa dau la pauni milioni 20 kwa Winga wa Uholanzi mwenye chini ya umri wa miaka 21 na winga wa Club Bruges Noa Lang, 22.
Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.


